Utawala wa
Kizayuni wa Israel umewahamishia gerezani watu wasiopungua 610 waliokuwa
kwenye meli zilizokuwa zikipeleka misaada ya kibinadamu katika eneo la
Ukanda wa Gaza. Taarifa zinasema kuwa, wafikishaji misaada na watetezi
wa haki za binadamu hao wamepelekwa kwenye gereza la Biirul Sab'aa
lililoko kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kabla ya hapo
viongozi wa utawala wa Israel walitangaza kuwa, ni watu 480 tu wa kutoa
misaada ya kibinadamu ndio waliopelekwa kwenye gereza hilo kwa ajili ya
kusailiwa na waliosalia hawajulikani walipo. Utawala huo ghasibu
umetangaza kuwa watu wengine 45 wengi wao wakiwa ni raia wa Uturuki
wamepelekwa hospitalini baada ya kupata majeraha yaliyosababishwa na
shambulio lililofanywa na makomandoo wa Kizayuni dhidi ya meli ya
misaada, na kusababisha watu 20 kupoteza maisha yao. Wakati huohuo, nchi mbalimbali duniani zimetoa radiamali zao kuhusiana na shambulio liliofanywa na Wazayuni dhidi ya meli za misaada ya kibinadamu. Kristen Halvorsen Waziri wa Elimu ambaye ni kiongozi wa mrengo wa kushoto wa chama cha Kisoshalisti nchini Norway ameitaka jamii ya kimataifa kuuwekea vikwazo vya biashara ya silaha utawala huo ghasibu.
Kiswahili Radio
|
Wednesday, June 2, 2010
Utawala wa Israel wawaweka jela watoa misaada ya kibinadamu
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Wednesday, June 02, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment