Wednesday, June 2, 2010
Rais Ahmadinejad: Jamii ya kimataifa ichukue hatua kuhakikisha mzingiro wa Gaza unaondolewa
Rais Mahmoud
Ahmadinejad amesema kuna ulazima wa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za
kuondoa mzingiro dhidi ya Gaza. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
ametoa mwito huo katika mazungumzo kwa njia ya simu aliyofanya na Ismail
Haniya, Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina. Katika mazungumzo
hayo, mbali ya kulaani shambulio la utawala wa kizayuni dhidi ya msafara
wa meli zilizobeba misaada ya kibinaadamu, Rais Ahmadinejad amesema
jamii ya kimataifa inapaswa kuanzisha harakati maalumu na kuongeza
maradufu juhudi zake za kuondoa mzingiro uliowekwa dhidi ya Gaza. Aidha
ametangaza kwa mara nyingine tena mshikamano wa taifa la Iran na
wananchi wa Palestina na kubainisha kuwa Iran inawaunga mkono kikamilifu
wananchi wa Palestina na wale wanaowaunga mkono wananchi hao. Wakati
huo huo shehena ya kwanza ya misaada ya kibinaadamu iliyotolewa na
wananchi wa Iran itasafirishwa hivi karibuni kwa ajili wananchi wa
Palestina wa eneo la Ukanda wa Gaza. Shirika la Hilali Nyekundu la
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuwa kufuatia mashauriano ya
kisiasa yaliyofanywa na viongozi wa Iran na nchi za eneo ikiwemo Misri
shehena ya kwanza ya misaada ya wananchi wa Iran inayojumuisha bidhaa za
vyakula, dawa na vifaa vya matibabu iko tayari kusafirishwa kuelekea
kivuko cha Rafah huko kusini mwa Gaza.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Wednesday, June 02, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment