BRAZIL NA KOREA KASKAZINI
Ushindi wa taabu wa mabao 2:1 wa mabingwa mara 5 wa dunia-Brazil
jana,umepokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Brazil nyumbani na hata
huko Afrika kusini na hasa uamuzi wa kumuacha nje ya kikosi cha
Selecao,Ronaldinho: Mashabiki wengi wamlaumu kocha Dunga wakidai
Ronaldinho, alistahiki kuwamo ndani ya kikosi hicho.
Ivory Coast na Ureno, ziliteremka uwanjani jana na kuondoka suluhu
0:0 huku majogoo wao 2-Cristiano Ronaldo na Didier Drogba, hakuna alitia
bao.
Hatahivyo, nahodha wa Ureno,Ronaldo, ndie aliepata nafasi bora kabisa
mnamo dakika ya 11 ya mchezo kutia bao,lakini mkwaju wake uligonga
mwamba wa lango la Corte d'Iviore.
Kwa vile, sasa Brazil, imeondoka na pointi 3 kwa kuishinda Korea mabao
2:1, Ivory Coast katika mpambano ujao na Brazil, itapaswa kujizatiti
barabara zaidi ,kwani, Korea ya kaskazini , imebainisha ni ngome nzito
kuitoboa.
New Zealand imetoka sare 1-1 na Slovakia kwenye mechi ya kundi F la Kombe
la dunia, katika uwanja wa Rustenburg
- Royal
Bafokeng.
Timu za taifa za New Zeland na Slovakia zashindwa kutambiana kwenye
michuano ya kombe la dunia baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1 kwa
1, katika mechi ya kundi F. Baada ya mechi ya New Zealand na Slovekia,
wawakilishi wengine wa Afrika, Ivory Coast ilimenyana na Ureno katika
mechi hiyo iliyokuwa ya vuta nikuvute, hadi dakika 90 za mchezo, matokeo
yalikuwa sare ya bila kufungana.
Wakati huohuo, watu wawili wameuawa na wengine 35 kujeruhiwa, baada ya kundi la waasi wa Hizbul Islam kuwashambulia mashabiki wa soka waliokuwa wakishuhudia fainali hizo kwa njia ya luninga karibu na Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. Wanamgambo wa kundi hilo waliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakiangalia mechi za kombe la dunia, na kusababisha kizaazaa kikubwa. Kundi hilo lenye misimamo ya kufurutu ada liliharamisha kuangalia mashindano ya kombe la dunia.

SVK
Robert
VITTEK alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo
0 comments:
Post a Comment