Tume iliyochunguza mauaji ya waumini 13 wa
kanisa Katoliki yaliyofanywa na wanajeshi wa Uingereza mwaka 1972
imebaini kuwa wanajeshi hao hawakuwa na haki kuwafyatulia risasi waumini
hao.
Uchunguzi wa tukio hilo lililojulikana kama
Bloody Sunday umeonyesha kuwa mmoja wa watu waliouawa alikuwa tishio.
Akitangaza matokeo ya uchunguzi huo katika bunge
la Uingereza waziri mkuu David Cameron amesema watu waliouawa au
kujeruhiwa walikuwa wakikimbia eneo la tukio au kuwasaidia wenzao.
Na hakuna hata mmoja aliyekuwa na silaha au
kuhatarisha maisha ya wanajeshi.
Cameron aliomba radhi kwa niaba ya serikali na
taifa akisema wanajeshi hawakutoa onyo lolote na baadae walisema uwongo
kuhusu kilichotokea.
Ripoti hiyo imetolewa baada ya uchunguzi
uliodumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.
Familia za marehemu zilifurahia uamuzi huo
wakisema wamesubiri kwa miongo kadhaa kupata ukweli.
Baadhi yao walirarua nakala za ripoti ya
uchunguzi wa awali ambayo ilisema jeshi la Uingereza halikuwa na hatia
yoyote.
0 comments:
Post a Comment