Mwenyekiti wa timu ya Azam Fc,Said Muhammad Said akiwa na mchezaji mpya wa timu hiyo,Mrisho Ngasa alietokea Yanga wakati akikabidhiwa uzi wake mpya leo katika makao makuu ya klabu hiyo.
Nyanda mpya wa timu ya Azam FC,Jackson Njovu akionyesha
uzi wake mpya mara baada ya kukabidhiwa leo na Mwenyekiti wa timu
hiyo,Said Muhammad Said.Nyanda Njovu alikuwa akiidakia timu ya JKT Ruvu.
Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC,Said Muhammad Said (kati) akiwa na wachezaji wake wapya,kushoto ni Mrisho Ngasa na kulia ni Jackson Njovu.

Wakati mchezaji Mrisho Ngasa akiamishwa kwa ada ya shilingi
milioni 58 kutoka timu yake ya zamani ya Dar Young African, timu ya Azam
imemnyakuwa kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove aliyekuwa amebakisha miezi
sita kumaliza mkataba wake na JKT Ruvu ambapo timu hiyo imeshamalizana
na uonozi wa JKT kwa kulipa kiasi cha shilingi milioni tatu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa wachezaji hao wapya Mwenekiti wa Azam Fc, Said Muhammad Said alisema kuwa baada ya kuwapata wachezaji hao lengo la klabu hiyo ambalo ni kuchukua Ubingwa wa ligi Kuu ya Vodacom katika msimu ujao.alisema "Wachezaji wazuri tunao hatuna sababu ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2010-2011".
Nae mchezaji mpya wa timu hiyo,Mrisho Ngasa alisema "Nitahakikisha timu yangu mpya inafanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,Najua kuna kila aina ya ushindani huko niendako lakini nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kiwango changu hakishuki na kuipatia Ubingwa wa Ligi Luu ya msimu ujao timu yangu mpya". aliongeza Ngasa.
Naye golikipa mpya wa timu hiyo aliyehamishwa kwa kitita cha shilingi milioni tatu kutoka JKT Ruvu, Jackson Chove alisema kuwa,baada ya kukosa kusajiliwa na timu hiyo katika msimu uliopita sasa amefika katika timu ambayo alikuwa anaipenda kutokana na kuwa na mapenzi na klabu hiyo tajiri hapa Tanzania. "Najua kama kuna ushindani mkubwa katika timu yetu lakini nitahakikisha nafanya mazoezi na kuongeza juhudi zaidi ili kiwango changu kisishuke" alisema Chove.

Michuzi.blogspot.
0 comments:
Post a Comment