SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 22, 2010

MEYA WA MWANZA KIZIMBANI KWA SHTAKA LA MAUAJI

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Leonard Bandiho Bihondo akiwasili Mahakama Kuu ya Mkoa wa Mwanza chini ya ulinzi mkali na pingu mikononi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Leonard Bandiho Bihondo akiingia chumba cha Mahakama.
Picha na Habari na Albert Sengo
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Leonard Bandiho Bihondo (64) amefikishwa katika Mahakama Kuu ya Mkoa wa Mwanza jana na kusomewa shitaka la kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya kada wa CCM Marehemu Bi. Bahati Stephano.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Mkoa, Yujnia Rujwahuka ndiye aliyemsomea mashtaka hayo. Kesi imeahirishwa hadi itakaposomwa tena tarehe 4 Juni 2010.
Bihondo. alikamatwa Jumatano jioni katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea jijini Dar es Salaam, amekuwa katika nafasi hiyo kwa miaka 10. Anahusishwa na maujai ya kiongozi wa CCM, kata ya Isamilo, Bi Bahati Stephano, aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani akiwa ofisini kwake Ijumaa iliyopita.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Silo ananukuriwa kusema kwamba katika upelelezi wa mauaji hayo, polisi waliwahoji washukiwa watatu, ambao wote alisema wamemtaja Bandiho kuwa amehusika katika tukio hilo.
Kuuwawa kwa kiongozi huyo wa CCM kumekuwa kukihusishwa na masuala ya kisiasa hususan uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mauaji hayo ambayo yamelitikisa jiji la mwanza yalielezewa na Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Laurence Masha kuwa ni ya kinyama na yalitokea saa chache baada kukutana na kiongozi huyo wa CCM.
Michuzi.blogspot

0 comments:

Post a Comment