Mawaziri wa
Fedha wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kwamba kuna
udharura wa kuwa imara zaidi kwenye bajeti zao hasa katika wakati huu
ambapo Ugiriki inakabiliwa na tatizo la madeni. Pia baada ya kukosolewa
kwamba nchi za Ulaya hazikuchukua hatua za kutosha ili kuilinda Euro,
mawaziri hao wameahidi kuchukua hatua za haraka zaidi na zenye athari
zaidi katika mustakbali kuhusu suala hilo. Herman Van Rompuy Mkuu wa
Kamisheni ya Ulaya amesema kuwa, nchi wanachama zimekubaliana juu ya
malengo muhimu manne, mojawapo ni kwamba wanapaswa kujiwekea vikwazo
vipya ili kuhakikisha sheria zinafuatwa. Wamesema kuwa, nchi ambazo
zitapata nakisi kubwa zaidi ya kiwango kilichowekwa kwenye bajeti zao,
zitaweza kupoteza haki ya kupewa fedha na nchi wanachama au kupoteza
haki ya kupiga kura. Katika siku za hivi karibuni, Euro imepungua
thamani na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kushuhudiwa katika
miaka minne iliyopita ikilinganishwa na dola.
Kiswahili Radio.
Kiswahili Radio.
0 comments:
Post a Comment