Chama tawala Kaskazini mwa Sudan
kimesema rais Omar Al Bashir amemteuwa raia wa eneo la Kusini kama
waziri wa mafuta katika jaribio la kuhifadhi umoja wa kitaifa.
Afisa mmoja wa chama tawala cha National
Congress Party, NCP, Ibrahim Ahmed Omar, ameiambia BBC kuwa hatua hiyo
inanuia kujenga imani baada ya juhudi za hapo awali za kuwahakikishi
raia wa eneo hilo la Kusini kuwa mapato ya taifa yanayotokana na mafuta
yatagawanywa kwa njia ya haki kushindwa kuzaa matunda.
Amesema chama cha NCP, kinatarajia kuwa uteuzi
huo wa raia wa eneo la Kusini kusimamia wizara muhumi, itawashinikiza
kupiga kura kupinga kugawanywa kwa taifa hilo mapema mwaka ujao.
Wakati huo huo Baraza jipya la mawaziri wa
serikali ya muungano nchini Sudan litaapishwa hii leo.
Baraza hilo lililotangazwa na rais Omar Al
Bashir hapo jana lina jumla ya mawaziri 77, 7 kati yao wakiwa wanawake.
Wabunge 3 kufikishwa mahakamani- Kenya
Malalamiko kuhusu wanasiasa hao yalitolewa na tume inayoshughulikia utangamano wa kitaifa nchini humo.
Mwenyekiti wa tume hiyo Mzalendo kibunja, anasema kuwa tume yake haina nguvu ya kuwachukulia hatua wabunge hao na hivyo watapelekwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao.
Inaripotiwa kuwa wawili kati yao walitoa matamshi hayo ya uchochezi wakati wa uzinduzi wa makao makuu ya wanaharakati wanaopinga rasimu hiyo ya katiba wiki mbili zilizopita.
Watatu naye anatuhumiwa kuwachochea wakaazi wa eneo lake la ubunge tarehe mosi mwezi huu.
Waziri wa Kilimo William Ruto ambaye anaongoza kundi wa wanasiasa wanaopinga katika hiyo inayopendekezwa anasema, serikali inawalenga ili kuwashurutisha kuunga mkono katiba hiyo.
BBC SWAHILI
Wabunge 3 kufikishwa mahakamani- Kenya
Wabunge watatu akiwemo waziri
mmoja wanatazamiwa kufikishwa mahakamani hii leo kujibu mashtaka ya
uchochezi.
Wabunge hao walitiwa nguvuni hapo jana na kulala
katika kituo cha polisi baada ya kutuhumiwa kutoa matamshi ya kueneza
chuki wakati wa kampeni za kupinga raasimu ya katiba mpya
inayopendekezwa.Malalamiko kuhusu wanasiasa hao yalitolewa na tume inayoshughulikia utangamano wa kitaifa nchini humo.
Mwenyekiti wa tume hiyo Mzalendo kibunja, anasema kuwa tume yake haina nguvu ya kuwachukulia hatua wabunge hao na hivyo watapelekwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao.
Inaripotiwa kuwa wawili kati yao walitoa matamshi hayo ya uchochezi wakati wa uzinduzi wa makao makuu ya wanaharakati wanaopinga rasimu hiyo ya katiba wiki mbili zilizopita.
Watatu naye anatuhumiwa kuwachochea wakaazi wa eneo lake la ubunge tarehe mosi mwezi huu.
Waziri wa Kilimo William Ruto ambaye anaongoza kundi wa wanasiasa wanaopinga katika hiyo inayopendekezwa anasema, serikali inawalenga ili kuwashurutisha kuunga mkono katiba hiyo.
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment