Milio ya makombora ya mizinga imeendelea kusikika, na machafuko kuanza upya huko nchini Kyrgzstan huku maelfu ya watu wanaokimbia mapigano ya kikabila yanayojiri nchini humo wakijaribu bila ya mafanikio kuvuka mpaka uliofungwa na kuingia nchi jirani ya Uzbekistan. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kumaliza machafuko huku wakitilia mkazo juu ya hatima ya wanawake, watoto na vikongwe ambao ndio wengi miongoni mwa watu wanaokimbia machafuko hayo. Mapigano mapya yamezuka huku serikali ya mpito ya Kyrgzstan inayoongozwa na Bi Roza Otunbayeva ikidai kuwa mapigano hayo yanamalizika na kusisitiza kwamba hakuna haja ya vikosi vya kusimamia amani kupelekwa nchini humo. Kwa mujibu wa takwimu za karibuni kabisa za Wizara ya Afya ya Kyrgzstan, watu wasiopungua 178 wameuawa na wengine 1,866 wamejeruhiwa kutokana na mapigano ya kikabila kati ya Wakyrgyz na Wauzbek yaliyotokea kwenye miji ya Osh na Jalalabad huko kusini mwa nchi hiyo. Hata hivyo Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema mamia ya watu wameuawa katika mapigano hayo. |
Wednesday, June 16, 2010
Machafuko yaanza tena Kyrgyzstan; hali ya kibinaadamu ni mbaya
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Wednesday, June 16, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment