Ivory Coast imetoka sare 0-0 na Ureno kwenye
mechi ya kundi G la Kombe la dunia, katika uwanja wa Nelson Mandela Bay
mjini Port Elizabeth.
Ivory Coast iliudhibiti mchezo lakini umaliziaji
wa Gervinho na Salomon Kalou ukakosa kuzaa matunda.
Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba
aliingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Salomon Kalou baada
ya shirikisho la soka duniani FIFA kumruhusu kufunga kifaa mkononi ili
kulinda jeraha lake.
Hata hivyo kuingia kwa Drogba hakukufanikisha
safu ya ufungaji, akibanwa na walinzi wa Ureno.
Awali katika mechi shuti la Cristiano Ronaldo
liligonga mwamba.
Mechi ya Ivory Coast itakayofuata itakuwa dhidi
ya Brazil siku ya Jumapili, kabla ya kumalizia michuano ya makundi dhidi
ya Korea Kaskazini tarehe 25.
Mlinzi wa Ivory Coast Kolo Toure aliondoka
uwanjani akichechemea baada ya kupata jeraha, na bado haijawa wazi ikiwa
ataweza kushiriki michuano itakayofuata.
Refarii Jorge Larrianda aliwaonyesha kadi ya
njano Cristiano Ronaldo na Guy Demel kwa kujibizana wakiambiana maneno
yasiyokubalika.
Kundi la G linaelezewa na wengi kuwa kundi la
'kifo' , kwani mbali na Ureno na Ivory Coast, linajumuisha mabingwa mara
tano wa kombe la dunia Brazil na Korea Kaskazini.
Vikosi
Ureno: Eduardo, Bruno Alves, Paulo Ferreira, Ricardo Carvalho, Cristiano Ronaldo, Pedro Mendes, Liedson, Danny (Simao Sabrosa, 55), Raul Meireles (Ruben Amorim, 85), Deco (Tiago, 62), Fabio Coentrao.
Mchezaji Christiano Ronaldo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
POR
0 comments:
Post a Comment