Wanachama wa baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa wamesema, kuna haja ya dharura ya kuhakikisha kuwepo
kwa maendeleo katika harakati za maandalizi ya kura ya maoni kuhusu
uhuru wa eneo la Sudan Kusini.
Akiongea na baraza hilo, afisa mmoja mwandamizi
wa Umoja wa Mataifa, amesema kuna hali ya wasi wasi kuhusu muda mdogo
uliosalia kabla ya kufanyika kwa kura hiyo ya maoni Januari mwakani.
Inatarajiwa kuwa raia wengi wa Sudan Kusini,
wataunga mkono kura hiyo na Umoja wa Mataifa umesema kazi ya kuchora
mipaka ya eneo la Kaskazini na Kusni imeanza pamoja na mpango wa
kugawana mapato yanayotokana na uuzaji wa mafuta.
Baraza hilo pia limeelezea wasi wasi wake kuhusu
kuongezeka kwa ghasia katika jimbo la Darfur Magharibi mwa nchi hiyo.
Takriban watu 500 waliuawa kwenye mapigano kati
ya jeshi la serikali na waasi katika eneo hilo mwezi uliopita.
Maelfu ya watu wengine wametoroka makwao katika
miezi ya hivi karibuni kukwepa mapigano hayo.
Rais Omar al Bashir wa Sudan aunda Baraza jipya la Mawaziri |
Rais Omar
Hasan al Bashir jana aliunda serikali mpya nchini Sudan ikiwa imepita
miezi miwili tangu ufanyike uchaguzi wa Rais nchini humo.
Habari kutoka Khartoum zinasema kwamba, Baraza jipya la Mawaziri la Sudan lina mawaziri 35 na nafasi nyeti kama vile Wizara ya Mambo ya Nje ameichukua Ali Karti kutoka chama tawala cha Congress ya Taifa. Rais al Bashir amemteua Lual Acuek Deng kutoka chama cha SPLM cha Sudan Kusini kuwa Waziri mpya wa Mafuta.
Mawaziri nane katika baraza hilo ni
kutoka kwa chama cha SPLM cha Sudan Kusini, 24 ni kutoka chama tawala na
watatu wengine ni kutoka vyama vitatu tofauti vya nchini Sudan.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2005 chama cha waasi wa zamani cha SPLM kilitiliana saini makubaliano ya mapatano na chama tawala cha Congress ya Taifa mjini Naivasha Kenya makubaliano ambayo yalikomesha miongo miwili ya vita vya kusini mwa Sudan. |
0 comments:
Post a Comment