Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mapambano
yanayosababisha damu kumwagika nchini Kirgistan.
Baraza hilo limetoa mwito wa kuumaliza mgogoro ulioikumba nchi hiyo
unaotokana na mvutano baina ya watu wa jamii za wakirgiz na
wauzbeki.Kwa niaba ya Baraza hilo balozi wa Mexico Claude Heller
ametoa mwito wa misaada kwa watu wa Kirgistan.
Tokea ghasia zianze nchini humo wiki iliyopita kutokana na mvutano
baina ya Wakirgiz na Wauzbek,ambao ni jamii ya wachache, watu zaidi ya
130 wameshakufa na wengine 1800 wamejeruhiwa.Maalfu wengine wamekimbilia
katika nchi jirani ya Uzbekistan.
Ili kukabiliana na matukio ya nchini Kirgistan Urusi kwa
kushirikiana na nchi za mfungamano wa ulinzi wa nchi zilizokuwa chini
ya himaya ya kisoviet zinafikiria kupeleka ndege aina ya helikopta na
magari.
Katibu Mkuu wa mfungamano huo OVKS, Nikolai Bordyusha amesema
Kirgistan ina majeshi ya kutosha lakini inahitaji zana zaidi za kijeshi. dw-world.d ***************** Mahakama ya ICTR yataka Nawukulilyayo ahukumiwe kifungo cha maisha |
Mahakama ya
Kimataifa ya Kufuatilia Jinai za Rwanda yenye makao yake mjini Arusha
Tanzania imetaka adhabu kali ya kifungo cha maisha itolewe dhidi ya
afisa mmoja wa Rwanda ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kuwaua kwa umati
maelfu ya Watutsi mwaka 1994.
Dominique Ntawukulilyayo mwenye umri wa miaka 68, alikuwa ni afisa wa kieneo wa mkoa wa Gisagara wakati yalipotokea mauaji ya kimbari nchini Rwanda na anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea, kuongoza na kufanya mauaji ya umati dhidi ya Watutsi wa Rwanda. Mahakama hiyo imesema kuwa, hakuna adhabu yoyote anayostahiki kupewa Ntawukulilyayo isipokuwa adhabu kubwa zaidi inayoweza kutolewa na mahakama hiyo nayo ni kifungo cha maisha. Mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni mwezi Oktoba 2007 nchini Ufaransa na inadaiwa kuwa alitumia gari lake kuwapeleka wanajeshi wa Kihutu kwenye maeneo ya milimani ili wakawamalize Watutsi ambao walikimbia mashambulizi ya raia wa Kihutu katika miji ya Rwanda mwaka 1994. Kiswahili Radio |
0 comments:
Post a Comment