Kiongozi wa chama kikuu cha
upinzani nchini Burundi ambaye zamani alikuwa kiongozi wa kundi la waasi
Agathon Rwasa ,amethibitisha kuwa yuko mafichoni.
Kwenye ujumbe uliorekodiwa na kutumwa kwa radio
moja nchini humo, Bw Rwasa amesema amejificha kwa kuhofia usalama wake.
Aliondoka nyumbani kwake wiki moja iliyopita
kabla ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumatatu huku mgombea pekee akiwa
Rais wa sasa Pierre Nkurunziza .
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza kufanyika nchini
humo,tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa
miaka 12.
Wanadiplomasia wameonya kuwa huenda nchi hiyo
ikarejea katika hali ya mzozo wa kivita.
Waandishi wa habari wanasema idadi ya watu
waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo wa urais, ilikuwa ndogo
ikilinganishwa na uchaguzi wa mikoa uliofanyika mwezi uliopita.
"Wananitafuta kwasababu nilisema ukweli,nilisema wazi kuwa sitakubali matokeo ya uchaguzi wa mikoa, walitaka kunikamata na nilipopata fununu nikaamua kukimbia"
Kiongozi wa chama cha
FNL Agathon Rwasa
Vyama vitano vya upinzani vilidai kuwa uchaguzi
huo ulikumbwa na wizi wa kura, na vikajiondoa katika uchaguzi wa urais.
Bw Rwasa, ambaye alitia saini mkataba wa amani
mwaka jana, hakusema yuko wapi lakini inaripotiwa kuwa yuko katika nchi
jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wakati alipotoweka kwa mara ya kwanza ,chama
chake kilisema alikuwa ''likizoni''.
Bw Rwasa na Rais Nkurunziza ,waliongoza makundi
ya waasi wa Kihutu kupigana na jeshi ambalo lilikuwa likiongozwa na
Watutsi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Bw Rwasa, alikataa kuhusika katika mpango wa kumaliza mapigano baada ya makundi yaliyokuwa yakizozana kuamua kuunda serikali ya muungano na baadaye uchaguzi ukafuata mwaka 2005.
Bw Rwasa, alikataa kuhusika katika mpango wa kumaliza mapigano baada ya makundi yaliyokuwa yakizozana kuamua kuunda serikali ya muungano na baadaye uchaguzi ukafuata mwaka 2005.
Aliongoza kundi la National Liberation Forces
(FNL) kusalimisha silaha mwezi Aprili mwaka 2009, na anaaminika kuwa
mshindani mkubwa wa Rais Nkurunziza.
Watu wapatao 300,000 walikufa wakati wa mapigano
ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
0 comments:
Post a Comment