Ripoti mpya imedokeza kuwa
maafisa wakuu wa kijeshi na wanasiasa nchini Zimbabwe, wanatumia ghasia
kuthibiti bishara ya Almasi.
Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika la Global
Witness, imesema mamia ya watu wameuawa katika eneo la Murange lenye
utajiri mkubwa wa madini ya almasi katika kipindi cha miaka mitatu
iliyopita.
Baadhi yao wanasema walipigwa, kubakwa na
kulazimishwa kuchimba madini hayo na wanajeshi na polisi wa nchi hiyo.
Ripoti hiyo inadi kuwa kampuni zilizoteuliwa na
serikali ya muungano nchini humo, kuimarisha hali ya wachimba migodi
yana uhusiano na rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, ambaye anazitumia kama
vyanzo vya fedha za kufadhili kampeini yake na chama chake cha Zanu PF.
Shirika hilo sasa limependekeza Zimbabwe
kuondolewa kama mojawapo ya nchi zinazoshiriki kwenye mazungumzo
yanayofanyika mjini Kimberley.
Mazungumzo hayo ya kimataifa yananuiwa kuzuia
uuzaji wa almasi inayokisiwa kusababisha mateso na maafa kwa raia.
0 comments:
Post a Comment