Tuzo yenye thamani kubwa duniani inayotolewa kwa
mtu binafsi, haitotolewa tena kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya
kuonekana hakuna anayestahili kushinda.
Mfanyabisahara wa Sudan Mo Ibrahim amekuwa
akitoa dola za kimarekani milioni tano kwa waliokuwa viongozi wa Afrika
kuhamasisha utawala bora katika bara hilo.
Amesema, " Viwango vilivyopangwa kwa mshindi wa
zawadi hiyo ni vya juu," akiongeza kuwa hakuna wagombea wapya walioibuka
tangu mwaka jana.
Washindi lazima wawe wamechaguliwa kwa misingi ya demokrasia na kukubali kuachia madaraka baada ya kukamilisha muda wake.
Washindi lazima wawe wamechaguliwa kwa misingi ya demokrasia na kukubali kuachia madaraka baada ya kukamilisha muda wake.
Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Olusegun Obasanja
wa Nigeria na John Kufuor wa Ghana ni miongoni mwa waliokuwa na sifa ya
kupata tuzo hiyo baada ya kuachia ngazi katika miaka mitatu ya awali.
Taarifa kutoka kwa wakfu wa Mo Ibrahim, " Ni
wazi kuwa itapita miaka kadhaa bila ya zawadi hiyo kutolewa. Mwaka
uliopita, hakuna wagombea wapya walioibuka."
Washindi hupokea dola za kimarekani milioni tano
kwa zaidi ya miaka 10, halafu dola 200,000 kwa mwaka mpaka atakapoaga
dunia.
Bw Ibrahim anasema zawadi hiyo inahitajika
kwasababu viongozi wengi kutoka nchi za bara la Afrika kusini mwa jangwa
la Sahara hutoka katika familia maskini na hivyo hushawishika
kung'ang'ania madaraka kwa hofu ya kurudi kwenye umaskini baada ya
kung'atuka.
Aliyekuwa Rais wa Botswana Festus Mogae
alishinda zawadi hiyo mwaka 2008 baada ya kukaa madarakani kwa mihula
miwili katika nchi hiyo yenye matukio machache ya rushwa na yenye
maendeleo.
Mshindi wa kwanza kabisa alikuwa Joaquim
Chissano, aliyekuwa Rais wa Msumbiji, ambaye tangu wakati huo amekuwa
mpatanishi wa migogoro katika nchi mbalimbali za Afrika.
Uchunguzi bado unaendelea kujua ni nani waliohusuka. Hata hivyo tayari makundi hasimu yameanza kuelekezeana lawama. Kundi la "NO" linalopinga katiba hiyo linadai kuwa huenda mlipuzi huyo alilenga kuhujumu mkutano wao na kulaumu polisi kwa kutotoa ulinzi wa kutosha kwao.
Waziri mkuu Raia Odinga hata hivyo amepuuza lawama hizo akisema kuwa kulikuwa na ulinzi wa kutosha. " Tusihusishwe na milipuko hiyo kwani sisi kama serikali hatuwezi kuruhusu raia waangamizwe. Kwani sio sisi tuliotoa kibali cha kufanyika mkutano huo?" aliongeza Raila.
Wakati huo huo, polisi wamegundua maiti ya mtu mmoja ndani ya gari aina ya Prado, aliyepigwa risasi na kuuawa mahali pa milipuko hiyo. Haijulikani iwapo kisa hiki kina uhusinao wowote na milipuko ya awali na tayari uchunguzi umeanzishwa. BCC SWAHILI
5 wauawa katika mlipuko mjini Nairobi
Nchini Kenya, Watu 5
wamethibitishwa kufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya
milipuko iliyotokea jana katika mkutano wa kupinga katiba mpya
inayopendekezwa.
Mkutano huo ulikuwa umepangwa na viongozi wa
kidini Mjini Nairobi na ulihudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo
wanasiasa. Polisi wanasema uchunguzi unaendelea na bado hawajui
kilichosababisha milipuko hiyo japo huenda ikawa bomu ya kujitengenezea
nyumbani.Uchunguzi bado unaendelea kujua ni nani waliohusuka. Hata hivyo tayari makundi hasimu yameanza kuelekezeana lawama. Kundi la "NO" linalopinga katiba hiyo linadai kuwa huenda mlipuzi huyo alilenga kuhujumu mkutano wao na kulaumu polisi kwa kutotoa ulinzi wa kutosha kwao.
Waziri mkuu Raia Odinga hata hivyo amepuuza lawama hizo akisema kuwa kulikuwa na ulinzi wa kutosha. " Tusihusishwe na milipuko hiyo kwani sisi kama serikali hatuwezi kuruhusu raia waangamizwe. Kwani sio sisi tuliotoa kibali cha kufanyika mkutano huo?" aliongeza Raila.
Wakati huo huo, polisi wamegundua maiti ya mtu mmoja ndani ya gari aina ya Prado, aliyepigwa risasi na kuuawa mahali pa milipuko hiyo. Haijulikani iwapo kisa hiki kina uhusinao wowote na milipuko ya awali na tayari uchunguzi umeanzishwa. BCC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment