SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 2, 2016

PROF. MBARAWA AKAGUA KIVUKO CHA MV. MALAGARASI, TTCL, POSTA NA KIWANJA CHA NDEGE MKOANI KIGOMA

Muonekano wa kivuko cha MV. Malagarasi kilichopo katika eneo la Ilagala mkoani Kigoma. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100, magari sita na tani 50 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), akipata maelezo ya kivuko cha MV. Malagarasi kutoka kwa Msimamizi wa Kivuko hicho kabla ya kukikagua. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani kigoma Eng. Narcis Choma na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na kuona namna ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akioneshwa vifaa vya uokoaji katika kivuko cha MV. Malagarasi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akijadiliana jambo na mmoja wa abiria wa Kivuko cha MV. Malagarasi.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS, mkoani kigoma Eng. Narcis Choma (wa tatu kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), barabara ya Simbo-Kalya yenye urefu wa zaidi ya Km 200 Kusini mwa Ziwa Tanganyika itakayoanza kujengwa hivi karibuni wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wananchi wa Ilagala, Sunuka, Karago, Herembe, Kapalamsenga, Mgambazi, Lukoma hadi Kashagulu ya namna sahihi ya kutumia kivuko cha MV. Malagarasi, mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akioneshwa namna ya huduma za uongozaji ndege zianvyofanyika katika kituo cha Kigoma. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole na katikati ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe akifatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole wakati alipokagua Uwanja wa Ndege mkoani hapo. Wa pili kulia ni Mbunge wa kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe akifatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia), wakati wa mkutano na wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa zao katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL) katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura.

0 comments:

Post a Comment