Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa
nyumba za Dege Eco Village zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius
Khyarara ametoa rai kwa wale Wote walionunua nyumba za Mtoni Kijichi
kukamilisha malipo ya nyumba hizo ndani ya siku 30 na kama hawatafanya
hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kunyang’anywa
nyumba na kuuzwa kwa wanachama wengine.
Mkurugenzi
Mkuu huyo alisema, wapo watu wameshikilia nyumba na hawajakamilisha
malipo kama mkataba unavyosema na kusisitiza kuwa ndani ya mwezi mmoja
kama mtu hajakamilisha malipo, masharti yote ya mkataba
yatafuatwa.Maagizo hayo aliyatoa wakati alipotembelea Miradi mbalimbali
ya NSSF Ukiwemo mradi wa Dege Eco Village.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara akifafanua jambo jijini Dar es Salaam, kuhusu wateja
walionunua nyumba za NSSF zilizopo Mtoni Kijichi kukamilisha malipo yao
ndani ya siku 30 kabla ya hatua za kisheria hazijachuliwa kwa
watakaoshindwa kufanya hivyo. Kushoto ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi
John Msemo.
Meneja
Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akitoa maelezo kuhusu mradi wa
ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
Godius Kahyarara.
Baadhi ya wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village.
Meneja
Kiongozi Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia)
akifafanua jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara
alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village Kigamboni
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara (kulia) akiangalia moja ya nyumba zilizopo katika mradi wa
Dege Eco Village.
Sehemu ya jikoni.
Nyumba za kisasa za Dege Eco Village.
0 comments:
Post a Comment