Mvua inayoendelea jijini Dar es Salaam Imesababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo.
Jambo ambalo limepelekea kufungwa kwa baadhi ya barabara.
1.Barabara ya Morogoro imefungwa maeneo ya Jangwani, kutokana na maji kujaa.
2.Kijitonyama, Temeke na pia Daraja la Salender imeezwa kuwa hali si shwari.
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum, Suleiman Kova anashauri watu kuondoka mjini mapema, ikiwa ni pamoja na kusikiliza maelekezo ya polisi wa barabarani.
Aidha, kama huna shuhguli ya msingi maeneo ya kinondoni, kariakoo, jangwani, muhimbili, upanga, posta, na maeneo ya karibu na hayo, usiende kwa siku ya leo, kwani kuna foleni kubwa.
Daraja la jangwani limejaa maji kiasi cha kufanya maji kupita juu ya daraja, jambo lililowafanya polisi kufunga barabara ya morogoro kuanzia mapipa hadi maeneo ya fire.
0 comments:
Post a Comment