SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, January 12, 2015

Padri John Wotherspoon atembelea tanzania kuonana na familia za walio magerezani kwa kukamatwa na mihadarati hong kong

Padri John Wotherspoon anayechapisha barua mbalimbali za 
wafungwa wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya Hong Kong.

Padri John Wotherspoon anayechapisha barua mbalimbali za wafungwa wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya Hong Kong baada ya kukamatwa na dawa za kulevya anafanya ziara nchini Tanzania kutembelea familia za wafungwa hao. Padri Wotherspoon alianza ziara yake mwishoni mwa mwaka jana na anaendelea na ziara ya kutembelea familia hizo hadi hivi sasa.

John Wotherspoon anasema aliwasili nchini akiwa na fedha za wafadhili kutoka Hong Kong kwa ajili ya kusaidia familia za wafungwa walio magerezani Hong Kong. Lakini fedha hizo zimeishia kwenye familia 5 tu huku bado akiwa na familia nyingine kama 30 za kutembelea na kuzijulia hali.

Padri huyo ambaye anayeendesha kampeni yake dhidi ya madawa ya kulevya kwenye tovuti yake ya Pope Francis amekuwa akichapisha barua nyingi kutoka kwa wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani huko Hong Kong baada ya kukamatwa na dawa za kulevya. Barua hizo zinapatikana hapa 2013).

0 comments:

Post a Comment