Mkurugenzi
wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga (kulia)
akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu safari
ya Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2013 kuelekea katika Mashindano ya Urembo
wa Dunia (Miss World 2014) nchini Uingereza.
Mshindi
wa Mashindano ya Urembo Tanzania kwa mwaka 2013, Happiness Watimanywa
(kushoto) akieleza jambo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam kuhusu safari yake ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika
Mashindano ya Urembo wa Dunia yatakayoanza mapema tarehe 14 Desemba,
2014.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kuhusu safari ya Miss
Tanzania 2013 nchini Uingereza kwenda kuiwakilisha Tanzania katika
Mashindano ya Urembo wa Dunia yatakayoanza mapema tarehe 14 Desemba,
2014. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM
***********
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
MREMBO
wa Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha
Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema
mwezi ujao huko nchini Uingereza.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo
amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa
akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya
hali na mali anayoipata toka Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani
wengine nchini amewaahidi Watanzania kuibuka na ushindi katika
kinyang’anyiro hicho huko nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
Alieleza
kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari
kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha
Tanzania katika mashindano hayo ya ulimbwende yatakayowahusisha
walimbwende toka Ulimwengu mzima.
“Nimejifunza
mambo mengi hasa kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini
pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo
nawaahidi watanzania ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko
Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
Naye
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga
ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo
wa Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende
toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa
watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye
ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili
ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
Mashindano
ya Urembo ya Dunia yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba,
2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia
kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014
tayari kwa ajili ya mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment