SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, November 12, 2014

Libya watatu wachinjwa kwa maoni yao


Mjini Derna, kundi la Is limeshika hatamu

Wanaharakati watatu wa kisiasa nchini Libya wamechinjwa baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya kiislam.Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna karibu na Benghazi.

Tukio hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu.Mji huo wa Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka 2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la is.

Mnamo mwezi August mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani katika viwanja vya mpira mjini Derna.

Siku za hivi karibuni kuna picha iloachiliwa mitandaoni ikionesha kikundi cha kijamii kinachojiita mahakama ya kiislam.


CHANZO: BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment