Mkuu
wa Huduma za Kibenki wa FINCA Tanzania, Bwana Gershom Mpangalah
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mradi wa
kusaidia vijana wa OYE unaofanywa kati ya FINCA na shirika la maendeleo
la SNV. Wanaotazama kutoka kushoto ni Mkuu wa Mradi OYE Upande wa Vijana
Bwana Awadh Milas, Mkuu wa Miradi ya OYE Tanzania, Mozambique na
Rwanda, Bwana Roy Van Der Drift na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Bwana Ed
Greenwood.
Na Mwandishi wetu
Shirika
la Maendeleo la Kiholanzi SNV na Mshirika wake Master Card Foundation
limezindua ushirikiano na FINCA M.F.C. Tanzania wenye lengo la kusaidia
vijana walioko nje ya mfumo wa shule katika mradi unaoitwa Fursa za
Ajira kwa Vijana (OYE) ambao utasaidia ajira kwa vijana zaidi ya 20,500
wanaoishi vijijini
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Mradi wa OYE Tanzania, Msumbiji na
Rwanda, Bwana Roy Van Der Drift, alisema ushirikiano baina ya SNV na
FINCA Tanzania ni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa OYE kwa miaka mitano
katika nchi za Tanzania, Msumbiji, Na Rwanda na utajikita katika kuwapa
vijana ujuzi kuhusu soko la fursa za ajira na kuwasaidia kuanzisha
biashara mpya.
‘Mahusiano
yetu na FINCA Tanzania yanalenga kutekeleza mradi wa OYE, na lengo kuu
ni kuhamasisha, kutia nguvu na kuhimiza vijana wa vijijini kubuni na
kubadilisha masoko yaliyopo na kutengeneza mapya” alisema Drift.
Ushirikiano
wa SNV na FINCA Tanzania, unalenga kuwawezesha vijana kufikia huduma za
kifedha, ushauri wa kibiashara na mafunzo yenye kuwajengea uwezo na
kujiamini na kuchangamkia fursa za masoko ya kilimo na nishati mbadala.
Mkuu
wa Miradi ya OYE Tanzania, Mozambique na Rwanda, Bwana Roy Van Der
Drift akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
“Biashara
ndogondogo zikiendelezwa zinaweza kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira
kwa vijana. Mradi huu utatengeneza ajira ambazo zitapunguza umasikini na
kuinua kipato miongoni mwa vijana waishio vijinini. Alisema Awadhi
Milasi, Mkuu wa Mradi OYE Tanzania upande wa vijana.
Mradi
wa OYE ambao uko katika mwaka wake wa pili kiutekelezaji umewapatia
mafunzo vijana Zaidi ya 1300 katika Nyanja za teknolojia, biashara ya
kilimo na nishati mbadala na unalenga kuwafikia vijana wengi Zaidi
katika elimu ya stadi za maendeleo ya biashara ambapo vijana wanaofikia
900 watapata mafunzo mwaka huu.
“Shirika
la kifedha la FINCA limekuwa mstari wa mbele kutoa misaada ya kifedha
kwa wajasiriamali wadogo kabisa na mpaka sasa linafanya kazi kwenye
mikoa 17 na matawi 26. Tuna uhakika kupitia Mradi wa OYE tutawafikia
vijana wengi zaidi na kutimiza ndoto zao za kibiashara” alisema Ed
Greenwood, Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA.
SNV
ni Shirika la Kimataifa la maendeleo linalofanya kazi katika nchi 35
kwa Africa, Asia na Amerika ya kusini. SNV inajenga uwezo wa serikali za
mitaa, vyama vya kiraia na mashirika binafsi katika kuendeleza masoko
ambayo yanajumuisha watu wasiojiweza katika kilimo, nishati mbadala na
maji safi.
0 comments:
Post a Comment