Vijana katika biashara ya uuzaji samaki.
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WAKATI
siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu kwa vijana watakao shiriki
Shindano la Mashujaa wa Kesho ukiwadia na dirisha la upokeaji fomu hizo
kutarajiwa kufungwa hapo kesho majira ya saa nane idadi ya vijana
waliorejesha fomu hizo imeendelea kupanda.
Akizungumzia
zoezi hilo jana mchana, Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil
Tanzania, Erick Mchome aliwataka vijana waliochukua fomu zao kuzirejesha
mapema ili kujipatia fursa ya kushiriki katika shindano hilo ambale
linaweza kuwakwamua vijana kiuchumi.
Vijana katika biashara ya uuzaji mapambo mbalimbali.
Akifafanua
zaidi, Erick Mchome alisema dirisha la kupokea fomu za Shindano la
Mashujaa wa Kesho linatarajiwa kufungwa rasmi kesho, Oktoba 10, 2014
majira ya saa nane za mchana na kuwataka vijana wachangamke kabla ya
muda huo kufungwa.
Alisema bado kuna idadi kubwa ya fomu ambazo hazijarejeshwa na vijana
waliochukua fomu hizo na kuwataka kufanya hivyo kabla ya muda wa zoezi
hilo kufungwa hapo kesho.
“Vijana
waliorejesha fomu mpaka leo (jana) ni takribani vijana 200. Waliochukua
fomu tangu siku ya uzinduzi Septemba 3, 2014 ni zaidi ya vijana 1000.
Hivyo natoa wito kwa vijana ambao bado hawajarejesha na wanataka kuingia
kwenye ushindani huu kurejesha fomu zao kwa wakati,” alisema Mchome.
Zoezi
zima la urejeshaji fomu litafikia tamati siku ya Ijumaa Oktoba 10, 2014
kabla ya saa nane mchana na baadaye kufanyika mchujo wa kupata vijana
40 watakaoingia hatua ya pili kabla ya kutangazwa washindi watano
ifikapo mwezi wa 12.
Aidha alivitaja vituo vya kurejesha fomu mkoani Mtwara kuwa ni pamoja na
Naliendele Agricultural Institute, Tanzania Institute of Accountancy,
VETA, Chuo cha Utumishi, Chuo cha Stella Maris Pamojana Pride FM.
Vijana katika biashara ya uuzaji samaki.
Naye
Mhadhiri wa Chuo cha Stella Maris ambaye pia ni Mratibu wa shindano hilo
kituo cha chuo hicho, Justin Lusasi aliwataka vijana kutokata tamaa
katika ushiriki kwani kitendo cha kushiriki pekee katika shindano hilo
na kuingia hatua ya pili ni faida kubwa kwao kwa kuwa watapata fursa ya
kujifunza jinsi ya kuaanda mipango ya biashara.
“Napenda
kuwasihi vijana wote warejeshe fomu zao, wala wasikate tamaa kwani kwa
kila atakayefanikiwa kuwa miongoni mwa washiriki 40 watakaoingia katika
hatua ya pili, atapata faida kubwa...watapata nafasi ya kujifunza
masuala ya biashara kama vile namna ya kuandika mipango ya biashara,
utekelezaji na usimamizi wa biashara,” alisema Lusasi.
Shindano la Mashujaa wa Kesho linaloendeshwa mkoani Mtwara linalenga
kuendeleza ujasiriamali kwa vijana mkoani Mtwara linaratibiwa na kampuni
ya uchimbaji gesi ya Statoil Tanzania.
Washindi
watano watapatikana ambapo mshindi wa kwanza atajishindia kitita cha
dola za Kimarekani 5,000 na dola 1,000 kwa washindi wengine wanne.
Washindi wanatarajia kutangazwa Desemba, 2014.
Vijana katika biashara ya ukaangaji na uuzaji samaki.
0 comments:
Post a Comment