SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, September 8, 2014

BENKI YA CRDB KUJENGA TAWI LA KISASA KATIKA KIWANDA CHA DANGOTE- MTWARA

  Ndege ya Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote ikiwasili katika uwanja wa Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), akiwa na balozi wa Nigeria, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mtwara, Francis Kasoyaga (wa pili kulia) wakiwa uwanja wa Ndege wa Mtwara wakati wakimsubiri kumpokea Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
  Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akishuka katika Ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mtwara.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akisalimiana na balozi wa Nigeria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akisalimiana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Mtwara, Francis Kasoyaga akipeana mkono na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
 Ujumbe ulioambatana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote ukifuatilia taarifa za kibenki kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa maelezo kuhusu uzoefu wa benki hiyo katika kuhudumia miradi ya kijamii kwa ujumbe ulioambatana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa maelezo kuhusu uzoefu wa benki hiyo katika kuhudumia miradi ya kijamii kwa ujumbe ulioambatana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akizungumza na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote. Katikati ni balozi wa Nigeria.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akiagana Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mishangu International, Godbless Kweka akipeana mkono na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Alhaji Aliko Dangote,akisalimiana na wenyeviti wa vijiji vinavyozunguka Kiwanda cha Dangote. 
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Benki ya CRDB litakalojengwa karibu na Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Kata ya Mayanga Mtwara Vijijini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akikata utepe kuzindua ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachojengwa jirani na Kiwanda cha Saruji cha Dangote ambapo gharama za ujenzi wa kituo hicho zitagharamiwa na mwekezaji huyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mishangu International, Godbless Kweka na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mishangu International, Godbless Kweka na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara wakifurahia baada ya uzinduzi huo.
Alhaji Aliko Dangote akisalimiana na baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB pamoja na waandishi wa habari kabla ya kumalizia ziara yake ya kutembelea kiwanda cha Saruji cha Dangote.
 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Kenneth Kasigila akiagana na Alhaji Aliko Dangote. 
NA MICHUZI MATUKIO

0 comments:

Post a Comment