Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida.
Pichani juu na chini malori mengine ya mizigo yakipita karibu na eneo la tukio.GPL(P.T)
Moja ya lori likitoa msaada wa kulivuta lori lililopata ajali kutoka bondeni.
DEREVA wa
lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea
Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo la Sekenke
mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo
wamejeruhiwa.
Mmoja wa
mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo
ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na
mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa
watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.
0 comments:
Post a Comment