Usitishaji wa muda mrefu wa mapigano umekubaliwa kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Kusitishwa kwa mapigano hayo, kumehitimisha wiki
saba za vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 2,200, wengi wao
wakiwa Wapalestina. Mazungumzo hayo yalisimamiwa na Misri na yalianza
kutekelezwa jana moja usiku.
Hamas wamesema mpango huo unawakilisha "ushindi wa upinzani wao".
Maafisa wa Israel wamesema Israel italegeza vikwazo ilivyoiwekea Gaza ili kuruhusu misaada na vifaa vya ujenzi kuingia Gaza.
Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas ametangaza kukubaliana na mpango wa kusitisha mapigano.
Msemaji wa serikali ya Israeli, Mark Regev
amesema: "hebu tuwe na matumaini kwamba mpango huu wa kusitisha mapigano
utaheshimika"
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika
masuala yenye utata, ikiwa ni pamoja na wito wa Israel wa kuyataka
makundi ya wapiganaji yanapokonywa silaha, yataanza mjini Cairo katika
kipindi cha mwezi mmoja.
Marekani imeunga mkono kikamilifu mpango huu,
kwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Psaki kusema:
"tunaunga mkono kikamilifu tangazo la kusitisha mapigano."
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia
amepongeza mpango huo wa kusitisha mapigano. Lakini katika taarifa
kupitia kwa msemaji wake, Bwana Ban ameonya kuwa "jitihada yoyote ya
amani ambayo haishughulikii chanzo halisi cha mgogoro, itafanya kazi
kidogo kuliko kutengeneza mzunguko mwingine wa ghasia".
Hatua ya kusitisha mapigano imekuja huku Israel na Wapalestina wakiendelea kushambuliana.
Kombora la dakika ya mwisho ya makabiliano
kutoka Gaza limemuua raia wa Israel na kuwajeruhi wengine sita katika
Barazala la Jimbo la Eshkol, wafanyakazi wa afya wameiambia BBC.
Mapema Jumanne, Wapalestina wapatao sita
waliuawa katika mfululizo wa mashambulio ya anga ya Israel huko in Gaza,
Wamesema maafisa wa Palestina.
Maafisa wa Palestina wamesema pendekezo la Misri
la kusitisha mapigano linataka kumalizwa kwa uhasama kusiko na kikomo,
kufunguliwa haraka kwa mipaka ya Gaza na Israel na Misri na kuongezewa
ukanda wa uvuvi katika bahari ya Mediterani..
Tangazo la kusitisha mapigano lilishangiliwa na Wapalestina katika mji wa Gaza.
Kabla ya kuanza utekelezaji wa mpango huo, majengo marefu mjini Gaza yalishambuliwa na makombora zaidi yalipiga Israel.
Mwezi mmoja baadaye Israel na vikundi vya
Wapalestina vitajadili ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege huko Gaza na
kuwaachilia huru wafungwa 100
Israel na Misri pia zimesemekana kutaka kuhakikishiwa kuwa silaha hazitaingizwa Gaza kwa njia ya magendo.
0 comments:
Post a Comment