Mgeni
rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP Mh. Mohammed Dewji (Mb) ambao
ndio wadhamini wakuu wa sherehe za uzinduzi wa jarida la IRIS Executive
(katikati), Ofisa Mtendaji Mkuu wa IRIS Executive Development Centre,
Phylisiah Mcheni (kulia) na Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Bw. Vipul
Kakad wakiwa meza kuu kwenye hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa jarida IRS
Executive ambalo tolea la jipya ukurasa wa mbele limepambwa na picha ya
Mh. Mohammed Dewji "MO".
Na Mwandishi wetu
OFISA
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP na Mbunge wa Singida Mjini kupitia tiketi
ya CCM, Mohammed Dewji, amesema kazi ya kutengeneza utajiri sio rahisi,
inahitaji mipangilio madhubuti na uvumilivu ili kufanikisha lengo hilo.
Mbunge
huyo ambaye kampuni zake zimeajiri watu 24,000 sawa na asilimia 5 ya
ajira rasmi nchini, amesema kutengeneza utajiri hakufanyiki kwa njia ya
kupanda lifti bali ni ujenzi wa tofali kwa tofali hadi nyumba
kukamilika.
Akiwa
anaendesha kampuni ambayo pato lake hadi mwishoni mwa mwaka huu
litakuwa ni za Marekani bilioni 1.5 amesema uwezo huo haukupatikana mara
moja bali umetokana na nia pamoja na kutrumia vyema fursa
zinazopatikana nchini.
Amesema
katika uzinduzi wa Jarida la IRIS Executive linalomilikiwa na Kituo cha
Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambacho kina ofisi
Tanzania, Kenya na wawakilishi nchini Uganda na Rwanda Vijana wa
Tanzania wapo katika nchi inayofaa na wakati muafaka na hivyo wanauwezo
mkubwa wa kutoka kiuuchumi.
Alisema
wakati uchumi wa afrika unakua kwa asilimia 5 na wa dunia kwa asilimia 8
uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 hali inayotoa nafasi kubwa kwa
vijana kusonga mbele ili mradi wachapekazi kwa bidii na maarifa.
Mhariri Mtendaji wa
jarida la IRIS Executive, Mike Mina akielezea historia fupi ya gazeti
hilo kwa wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa
jarida hilo ulifanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Dar Es
Salaam Serena. Kushoto ni Meneja Masoko wa jarida la IRIS Executive,
Alinda Henry.
Katika
uzinduzi wa jarida hilo lenye nakala 40,000 mtaani katika nchi zote za
Afrika Mashariki na likizingatia mahitaji ya ukuaji wa uchumi Afrika
Mashariki, Dewji maarufu kama Mo amewataka vijana kuhakikisha kwamba
wanatoa habari kwa haraka na kwa muda muafaka kwani ndio kichochea cha
uwekezaji na uendeshaji.
Alikubaliana
na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo Mike Mina kwamba habari ni kitu
muhimu katika kufanikisha uwekezaji na biashara, lakini akasisitiza
habari zinaoztolewa katika muda muafaka.
IRIS
Executive ambalo katika toleo lake la pili limeandika habari kumhusu Mo
ambaye kwa miaka 15 amefanikiwa kuiondoa MeTL kutoka pato la dola
milioni 30 hadi dola bilioni 1.5,huandika na kufuatilia masuala ya
maendeleo hasa katika sekta zinazogusa uchumi moja kwa moja kama fedha
na benki, uzalishaji viwandani, mafuta na gesi, kilimo na uwekezaji.
Toleo lake la kwanza lilimgusa Ofisa Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi.
Akizungumza
historia yake kabla ya kuzindua jarida hilo alisema kwamba yeye
alizaliwa nyumbani na mkunga wa kienyeji 1975 kama walivyo watanzania
wengi na kwamba amefikia hapo kwa bidii kubwa akitaka vijana kuiga
safari hiyo kwa kutumia vyema fursa zilizopo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development
Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni
akizungumza na wageni waalikuwa kwenye uzinduzi huo.
Kampuni
ya MeTL inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo
na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara,
petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na
masuala ya simu.
Aidha
kampuni hiyo inajivunia kufanya biashara katika nchi za Ethiopia,
Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan
Kusini na Kenya huku ikiwa na viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee.
Dewji
amepata elimu ya juu kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani
ambacho katika baadhi ya maelezo yake anasema ndio iliyomfumbua macho na
kuona umuhimu wa kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani.
Mara
nyingi MO amekuwa akisema,Falsafa yake kama mfanyabiashara sio
kuridhika na mafanikio aliyonayo bali kuendelea kufanyakazi kwa bidii na
kufanikiwa zaidi. Alisema.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) ambao ndio
wadhamini wakuu wa sherehe za uzinduzi wa jarida la IRIS Executive
akitoa nasaha zake kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa jarida hilo usiku wa
kuamkia leo katika hoteli ya Dar es Salaam Serena.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu- IRIS Executive Development Center, Phylisiah
Mcheni akimkaribisha MO kuzindua jarida hilo, pamoja na kumshukuru kwa
kudhamini uzinduzi huo pia alisema, IRIS Executive ni jarida pekee lenye
makazi yake nchini Tanzania kuweza kufika nchi zote za Afrika Mashariki
kwa idadi za nakala na taarifa zilizomo ndani zinazolenga uwekezaji na
biashara kwa watendaji ni matumaini yetu kwamba wasomaji watakuwa siku
zote wanajua nini kinachoendelea kwa manufaa yao, makampuni na sekta
mbalimbali zinazochangia katika kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na
taifa.
Aidha pamoja na kulipata jarida hilo la IRIS Executive katika nakala halisi pia hupatikana katika mtandao kwa anuani ya www.irisexecutive.com
Uzinduzi
huo ulihudhuria na maofisa watendaji wa ngazi mbalimbali kutoka
makampuni yanayojishughulisha na uwekezaji,biashara, habari na
utamaduni.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni (kulia) akiitambulisha timu yake ya vijana na jarida hilo kwa wageni waalikwa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni wakijiandaa kuzindua rasmi jarida hilo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akizindua
rasmi jarida hilo huku ukurasa wa mbele ukiwa umepambwa na picha yake
sambamba na mahojiano maalum aliyoelezea mafanikio na changamoto
mbalimbali alizopitia katika biashara hadi hapo alipofika. Kushoto ni
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni akishuhudia tukio hilo.
|It's now official launched".....Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni wakifurahi pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa jarida hilo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akikata keki maalum iliyoandaliwa kusindikiza uzinduzi huo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akimlisha
kipande cha keki Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike
Mina.
Mgeni
rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb)
akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa jarida la IRIS Executive.
Kutoka kushoto ni Ofisa uhusiano na raslimaliwatu wa IRS Exexcutive, Beatrice Silayo, Jokha Sadiki, Ofisa Mtendaji Mkuu waKituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb),Mhariri Mtendaji wa
jarida la IRIS Executive, Mike Mina, Meneja Masoko wa jarida la IRIS
Executive, Alinda Henry na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Fedha wa
jarida la IRIS Executive Bw. George Saltai.
Mjumbe
wa halmashauri kuu CCM (NEC) na Katibu wa Mbunge wa Singida mjini,
Hassan Mazala (kulia) naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
Katikati ni Ofisa anayeshughulikia masuala ya Fedha wa jarida la IRIS Executive Bw. George Saltai.
Picha juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa jarida la IRIS Executive na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Meneja
Mkazi wa Shirika la Ndege la Rwanda, Hafeez Balogun (kushoto) na Meneja
Mauzo wa Shirika la Ndege la Rwanda, Dhruv Parmar (katikati) pamoja na
Meneja Mkuu wa African Life Assurance, Bw. Wilson Mnzava (kulia)
wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye halfa hiyo.
Msaidiz
wa Mh. Mohammed Dewji "MO" Nicole Cherry akipiga picha matukio
mbalimbali kupitia simu yake ya kiganjani wakati wa hafla hiyo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development
Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni
akibadilishana mawazo na Meneja
Mkazi wa Shirika la Ndege la Rwanda, Hafeez Balogun (katikati) na
Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege la Rwanda, Dhruv Parmar (kushoto)
kwenye sherehe za uzinduzi wa jarida hilo.
Meneja
Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia)
akibadilishana mawazo na Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive,
Mike Muna wakati wa uzinduzi wa jarida hilo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development
Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah
Mcheni (wa pili kulia) katika picha na mmoja wa wageni
waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa jarida la IRIS Executive
ambalo kwa sasa liko mitaani na unaweza kujipatia nakala yako.
Mbunifu
wa Mavazi nchini Tanzania, Sheria Ngowi akisalimiana na Meneja Mkuu wa
African Life Assurance, Bw. Wilson Mnzava wakati wa uzinduzi wa jarida
hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe (kulia)
akisalimiana na Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Sheria Ngowi kwenye
hafla fupi ya uzinduzi wa jarida la IRIS Executive uliofanyika usiku wa
kuamkia leo.
Mbunifu
wa Mavazi nchini anayefanya vizuri katika soko la kimaifa Sheria Ngowi
(kulia) akiwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko cha Sheria Ngowi Brand,
Deogracious Kessy wakati wa uzinduzi wa jarida la IRIS Executive.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
0 comments:
Post a Comment