Msichana wa kazi za ndani, Fonolia Lembres (12) aliyeshambuliwa kwa mapanga na tajiri wake, Emmanuel Msovera.
Na Joseph Ngilisho, Arusha
Fonolia ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mount-Meru,
jijini hapa, amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto
na maeneo mengine ya mwili kisa kikidaiwa kuwa ni kutuhumiwa kuiba
shilingi 30,000 za bosi wake huyo.
Hata hivyo, majirani na nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wameeleza kuwa
msichana huyo amekuwa akipigwa kama mbwa mwitu kila siku kiasi cha wao
kumtaka mtuhumiwa amrejeshe kwao iwapo ameshindwa kukaa naye.
Akizungumza kwa tabu akiwa hospitali alikolazwa , mfanyakazi huyo wa
ndani alilalamika kutoona vizuri kutokana na jicho lake la kushoto
kupigwa ngumi pia maumivu makali ya mkono pamoja na sehemu zingine
alizokatwa kwa panga na fyekeo.
Akisimulia tukio hilo alisema, mke wa mtuhumiwa, Rose Benjamini, mumewe
alimchukuwa binti huyo kwa wazazi wake miaka minne iliyopita kwa
makubalino ya kumsomesha lakini badala yake akawa anampiga mara kwa
mara.
Alisema maisha yake yote yamekuwa ya mateso makubwa kwani amekuwa
akipigwa na kunyanyaswa kwa kiwango kikubwa na wakati mwingine hata
kunyimwa chakula ambapo alikuwa akivumilia mateso hayo.
Alisema siku ya tukio (Jumamosi iliyopita) usiku majira ya saa tatu,
Benjamini ambaye ni kondakta wa Hiace zinazofanyakazi kati ya mjini na
kwa Morombo, alifika na kumuuliza kuhusu fedha zake kiasi cha shilingi
elfu 30 alizoziacha kwenye kochi.
“Nilimwambia sikuchukua ndipo alichukuwa panga na kunikata mkono,
baadaye alichukuwa fyekeo na kunikata mguuni na sehemu zingine na
kunipiga ngumi kwenye jicho,’’ alisema mwanafunzi huyo.
Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio
hilo walitoa taarifa kwa balozi wa eneo hilo, Joseph Mtinangi ambaye
alichukuwa jukumu la kutoa taarifa polisi ambao walifika na kumkuta
mtuhumiwa amejifisha
juu ya dari katika chumba chake, wakamkamata na kumfikisha kituo kikuu cha polisi jijini hapa.
Mtuhumiwa huyo amefunguliwa hati ya mashitaka yenye kumbukumbu namba
AR/RB/10071/2014 KUJERUHI.Kwa upande wake balozi Mtinangi alilaani tukio
hilo na kueleza kuwa ni tukio la kinyama ambalo mtuhumiwa amekuwa
akimtendea mara kwa mara msichana huyo.
Aliongeza kuwa alikuwa akipata malalamiko juu ya tukio hilo ambapo
aliwaonya wahusika lakini kwa kitendo alichokifanya siku hiyo ametoa
wito kwa vyombo vya dola kuchukuwa hatua kali ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
0 comments:
Post a Comment