Liverpool imekubali kumuuza mshambulizi wake Luis Suarez kwa Barcelona kwa kima cha pauni milioni 75.
Mchezaji huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka ,
27, ambaye amepigwa marufuku ya miezi miinne kwa kumuuma mchezaji
mwenzake wa Italy, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao katika kombe la
dunia, atasaini mkataba wa miaka mitano.
Suarez, ambaye aliingiza mabao, 31
katika ligi ya premier msimu uliopita, atasafiri kwenda Uhispania wiki
ijayo kwa uchunguzi wa kimatibabu.
"Luis ana kipaji cha kipekee, na ninamshukuru kwa alivyotuwakilisha,'' alisema meneja wa Liverpool Brendan Rodgers.
Suarez anasema kuwa yeye pamoja na familia yake, daima watakuwa mashabiki wa Liverpool.
Suarez alikuwa mfungaji mabao mengi zaidi katika
msimu uliopita na mshindi wa tuzo la mchezaji bora . Alitia saini
mkataba na Liverpool alipotoka Ajax mwaka 2011 kwa pauni 22.7.
Alikuwa amesalia na miaka minne katika mkataba wake.
Hatua ya Suarez kuhamia Barcelona inampeleka karibu na mkewe pamoja na familia yake.
"Ni kwa majonzi mengi nimeamua kuondoka
Liverpool, kwa maisha mapya nchini Uhispania na cha mno ni kwamba
nimefurahishwa sana na mashabiki, '' alisema Suarez
"Ninatumai nyote mtaelewa uamuzi wangu. Klabu
hii ilinifanyia kila nilichokitaka, lakini kucheza na kuishi uhispania,
ilikuwa ndoto yangu kubwa. Muda huu uko sawa sana kwangu. ''
"Ninamtakia Brendan Rodgers na kikosi chake kila
la heri na mustabali mwema. Klabu hiyo iko chini ya usimamizi mzuri na
pia natumai watafanikiwa msimu ujao.''
0 comments:
Post a Comment