SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 18, 2014

WAZIRI WASSIRA KATIKA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaack Nantanga akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kushoto) katika Banda la Wizara hiyo, kupata taarifa mbalimbali za Muungano zinazotekelezwa na wizara hiyo pamoja na taasis zake. Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Thomas William (kushoto) akimfafanulia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kulia) jinsi mamlaka hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jinsi inavyofanya kazi zake Tanzania Bara na Visiwani. Waziri Wassira alilitembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonesho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
 Ofisa wa Jeshi la Polisi, Christina Mponji akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (wa pili kushoto) picha za Wakuu wa Jeshi la Polisi mbalimbali toka tulipopata uhuru hadi wa hivi sasa.  Waziri Wassira alilitembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambalo lina Taasisi tatu za Muungano ambazo ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Maonesho hayo ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaack Nantanga (kushoto) akigawa vipeperushi mbalimbali za wizara hiyo kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Taasisi zake za Muungano ambazo ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kushoto) akipokea vipeperushi vya Idara ya Uhamiaji alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Taasisi zake za Muungano katika  Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).