Waziri
wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Chikawe (kushoto) akipokea ufungua wa gari
kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Joyce Mends-Cole. Gari hiyo ambayo ni mpya aina ya Toyota
Land Cruiser imetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kusaidia shughuli
mbalimbali za kiutendaji zifanywazo na Idara ya Wakimbizi nchini iliyopo ndani
ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika
katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiifurahia gari mpya aina
ya Toyota Land Cruiser baada ya kukabidhiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole
(kushoto).
Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani.