Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Mkurugenzi wa
Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alipowasili katika hoteli ya Ledger
kuhudhuria semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau na wawekezaji katika sekta ya fedha.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Katibu wa Benki ya CRDB.
Naibu Waziri waFedha na Uchumi, Kigoma Malima akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima (kushoto), akiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau na wawekezaji katika sekta ya fedha.
Tunafuatilia mkutano......
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa mada wakati wa
semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam,
na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa
semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam
na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akifungua semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Washiriki na wadau wa semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akifuatilia kwa makini semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa
mada wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es
Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akiteta jambo ma
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima.
Naibu
wa Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya uwezekezaji ya
Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kufungua semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Kigoma Malima akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wawekezaji katika sekta ya fedha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina ya uwekezaji ya Benki ya CRDB iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa wakurugenzi ya Benki ya CRDB. Martin Mmari akizungumza na waandishi wa habari.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imezitaka benki nchini kupanua huduma za kifedha kwa wananchi ili
kuweza kufanikisha ukuaji wa uchumi kwa maendeleo ya Taifa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa
taarifa za kifedha kwa wadau na wawekezaji kwenye sekta ya fedha benki ya CRDB, Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima alisema, watanzania wanaonufaika na huduma za benki
ni wachache lakini huduma za kifedha ni wengi hivyo kupanua wigo utaongeza
upatikanaji wa fedha kwa urahisi.
Alisema sekta ya benki inamchango mkubwa katika kukuza
uchumi wa nchi na kuleta maendeleo na ndo maana CRDB imeweza kuwaita wawekezaji
wengi ili kuwekeza kwenye sekta muhimu ya fedha na yenye tija katika jamii .
“Jambo kubwa na la muhimu tunataka watanzania waweze
kunufaika na huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa, wajibu wenu sasa CRDB
kuendelea na utafiti ili kujua ni kwa namna gani mtaweza kuwafikia watu wengi
zaidi katika huduma hizi za kibenki zenye lengo la kukuza uchumi wa nchi,”
alisema.
Aidha alisema pamoja na uchumi wa Dunia kuteteleka lakini
Tanzania aikuteteleka hiyo ni kutoka na kuwa na huduma bora na za uhakika
zinazotolewa na benki hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dk. Charles
Kimei, alisema utoaji wa taarifa za kifedha pamoja na uchambuzi wa
kina unasaidia kuona muelekeo wa benki jinsi ulivyo hivyo wameamua kukalibisha
wawekezaji wengi katika soko la hisa ili kuweza kukuza uchumi.
“Mwaka huu tumekaribisha wawekezaji wengi zaidi kwenye soko
la hisa hiyo ni kwasababu mwaka jana tulifanya vizuri na kuingiza faida nyingi
hata hivyo rasilimali za benki zimekuwa kwa asilimia 17 na bado zinaendelea
kuongezeka zaidi,” alisema
Alisema uwongezekaji wa faida unatoka na kuwa na mazingira
mazuri ya kiuchumi na wateja kukubali huduma za kibenki kwani uhamini zaidi
huduma zao na kuzipenda.
NA ANKAL MICHUZI