Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea maelezo
kutoka kwa Afisa wa Bunge Bwana Patson Sobha, wakati alipowasili kwenye
Banda la Bunge la maonesho ya maadhisho ya miaka 50 ya Muungano wa
Tanzania yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Maonesho hayo yatakayofikia kilele siku ya Jumamosi Aprili 19, ikiwa ni
maandalizi ya siku kuu ya Muungano ambayo huherekewa Aprili 26 kila
mwaka.
Rais
Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya vitabu na
nyaraka mbalimbali za Bunge na Bi. Devotha George alipotembelea banda la
Ofisi ya Bunge kwenye Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano
katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
ais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye
ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea
katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka
katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya sherehe za
Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu
wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akimsikiliza kwa makini Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles
Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo katika
Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.