SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 26, 2014

NSSF YATOA SEMINA KUHUSU MAFAO NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU KWA MAOFISA UTUMISHI RAS, DED NA MANISPAA

 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Crescentius Magori akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu mafao na utunzaji kumbukumbu kwa  maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa kutoka mikoa yaote ya Tanzania Bara. Semina hiyo imeandaliwa na NSSF na kufanyika leo Mkoani Morogoro. Wa pili kushoto ni Ofisa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Crescentius Magori akitoa mada kuhusu mafao ya muda mrefu ya pensheni ya uzeeni, Pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi pamoja na mafao ya muda mfupi ambayo ni mafao ya matibabu, mafao ya kuumia Kazini, mafao ya uzazi na msaada wa mazishi. Semina hiyo iliandaliwa na NSSF kwa ajili ya maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
 Mshiriki wa semina ya maofisa utumishi wa manispaa akisoma kipeperushi cha taarifa za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kabla ya kuanza kwa semina ya maofisa utumishi ilifanyika mjini Morogoro na kuandaliwa na NSSF.
 Maofisa wa NSSF wakiwa katika semina hiyo.
 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza maswali.
 Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada.
 Baadhi ya maofisa Utumishi wakiwa katika semina hiyo.
 Meneja wa NSSF anayeshughulika na Idara za Serikali na Ofisi za Balozi, Rehema Chuma (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa.
 Mshiriki kutoka Kigoma akichangia mada katika semina hiyo.
Maofisa wa NSSF wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Uendesha wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina kuhusu mafao na utunzaji kumbukumbu kwa  maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Mkurugenzi wa Uendesha wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina kuhusu mafao na utunzaji kumbukumbU kwa  maofisa utumishi RAS, DED na Manispaa iliyofanyika leo mjini Morogoro.