SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 25, 2014

Top 20 ya 'Mama Shujaa wa Chakula' watakaoingia kijiji cha Maisha Plus wikiendi hii


GRACE G.D MAHUMBUKA (46) mkazi wa Karagwe Kagera nambari yake ya ushiriki ni MS 08, ni mkulima wa shamba la ekari 18 na na mfugaji wa ng’ombe, kondoo na mbuzi.


ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anawahamasisha wana kijiji kutumia vyema mvua za kwanza na kupanda miti kwa ajili ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kutunza mazingira."Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 18. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 35"

NEEMA URASSA KIVUGO (48) (Mshindi: Mama Shujaa wa Chakula Mtandaoni) ni mkazi wa Kiteto Manyara, namba yake ya ushiriki ni MS 12, na mkulima wa shamba la ukubwa wa ekari 10. 

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Yeye ni mchapakazi na anachukulia kilimo kama njia ya kumkwamua dhidi ya umasikini. Yeye ni mbunifu na hujifunza kwa haraka. Anavuna mazao gunia 78 kwa mwaka.

MARY JOHN MWANGA (52) ni mkazi wa Mkalama Singida, ni mkulima na mfugaji anashamba la ekari 5 na analima mahindi na anafuga ng’ombe watano

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anashiriki katika shughuli za maaendeleo ya kijiji, michango na mikutano. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 22" anasema
DORICUS MSAFIRI SHUMBI (38) namba yake ya ushiriki ni MS 25 ni mkazi wa Mkalama Singida, mkulima na mfugaji, ana shamba la ukubwa wa ekari 5 ambayo anaitumia kulima mahindi, anafuga ng’ombe 5.
ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anapenda kujitoa na kushirikiana na vikundi mbalimbali "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 7. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 56" anasema

KURUTHUMU RAMADHANI MWENGELE (48) namba yake ya ushiriki ni MS27, ni mkazi wa Korogwe Tanga na ni mkulima na mfugaji analima ekari 6 na anafuga kuku 6, mbuzi 6 na bata 4.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anashirikiana na wenzakekupeana mawazo kwa ajili ya ufugaji bora na kilimo cha kisasa. "Kwa mwaka ninavuna hoho 8,000 na tango 7,000" anasema

MARY ATHANAZ NDASI (38) mkazi wa Sumbawanga Rukwa namba yake ya ushiriki ni MS 21 yeye ni mfugaji wa kuku.
ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu kutokana na mradi huu ameweza kujenga na kulipa karo za shule za watoto na familia inapata chakula cha kutosha. Anasema "Kwa mwaka ninapata trei 4,320 za mayai"

SANTINA MAPILE (27) mkazi wa Njombe namba yake ya ushiriki ni MS 20 ni mfugaji na anafuga nguruwe.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu amewahi kupata mafunzo ya ujasiriamali na akabahatika kupata mkopo na kurejesha kwa wakati. Anasema "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 1.5. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 15"

THEREZA KITINGA (44) mkazi wa Sengerema Mwanza namba yake ya ushiriki ni MS 18, ni mkulima wa shamba la ukubwa wa ekari 10.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anazingati ataratibu za kilimo cha kisasa na anshirikiana na wenzie kuzalisha mazao mengi ili kujihakikishia chakula kingi. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 10. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 80"

NEEMA GILBERT UHAGILE (28) mkazi wa Njombe namba yake ya ushiriki ni MS 19 ni mkulima na mfugaji ana ekari 2 anazolima mahindi, maharagwe na maparachichi na anafuga kuku na ng’ombe.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anapenda kazi ya kilimo  na ufugaji na pia anajiamini katika kazi yake.Anasema "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 10 na ninapata mayai trei 200"

FREDINA M SAID (43) mkazi wa Kishapu Shinyanga namba yake ya ushiriki ni MS 22 ni mkulima na ana sahamba lenye ukubwa wa ekari 12.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anabuni njia mbalimbali za kumuingizia kipato na pia anaunda vikundi vya kijasiriamali na anaendesha mdahalo kwa wanawake ili wajitambue. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 67" anasema

ESTHER KULWA (57) mkazi wa Simiyu namba yake ya ushiriki ni M 23 ni mfugaji na mkulima na ana shamba la ukubwa wa ekari 7 anazotumia kulima mpunga na mahindi, pia anafuga ng’ombe 7.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababuanahamasisha akina mama kuwa wajasiriamali kupitia kilimo na kupata mitaji. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 90" anasema

JOYCE NORMANI HASSAN (44) mkazi wa Masasi Mtwara nambari yake ya ushiriki ni MS 16 ni mkulima na ana ekari 2 za mahindi, korosho na mbogamboga.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anaendesha kilimo cha kitaalamu na pia amejiunga na vikundi mbali mbali. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 6. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 27"

ELIZABETH SIMON mkazi wa Kilosa Morogoro namba yake ya ushiriki ni MS 15 ni mkulima wa mahindi na mpunga ekari 2 na mfugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anajishughulisha na kilimo. "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 20 na ninapata lita 5,000 za maziwa"

ZINAIDA JAMES KIJERI (40) mkazi wa Kakonko Kigoma, namba yake ya ushiriki ni MS 10, ni mkulima wa shamba la ukubwa wa ekari 7 na mfugaji wa ng’ombe 10 na mbuzi 15.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu anajiamini na anajituma katika shughuli mbalimbali na pia kushauriana na wafugaji wengine pamoja na wakulima. Anasema "Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 30 na ninapata lita 1,825 za maziwa"

ELINURU MOSES PALLANGYO (52) mkazi wa Meru Arusha, namba yake ya ushiriki ni MS 01, ni mkulima na mfugaji ana shamba la ukubwa wa robo tatu ekari, analima ndizi na mboga na kufuga ng’ombe, mbuzi na kuku.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Anajituma na kazi yake inaonekana, watu kutoka ndani na nje ya nchi, vikundi, mashirika naa watu binafsi huwenda kujifunza katika darasa lake la kujitolea.Anasema "kwa mwaka ninavuna ndizi mikungu 70, ninapata kilo 336 za nyama za kuku pamoja na maziwa lita 3780"

LEAH DOMINICK MNYAMBUGWE (52) mkazi wa Dodoma Mjini namba yake ya ushiriki ni MS 03, yeye ni mkulima na mfugaji ana shamba la ukubwa wa ekari 21.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu mifugo insaidia kupata kipato pia kuelimishana kuhusu ufugaji wa kisasa na kupata mazao bora. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 21. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 40 na ninapata lita 1,460 za maziwa"

DOROTHY DANIEL PALLANGYO (64) mkazi wa Meru Arusha, namba yake ya ushiriki ni MS 02 yeye ni mkulima na mfugaji ana shamba la ukubwa wa ekari 2 na anafuga ng’ombe na mbuzi.
ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA:  Kwa sababu Anafuga kisasa na ana banda bora la mifugo, pia analima kwa kuotesha kwa kufuata ushauri wa kitaalamu. "nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 30 na ninapata lita 5,040 za maziwa"
UPENDO MBAZI MSUYA  (38) ni mkazi wa Mwanga Kilimanjaro nambari yake ya ushiriki ni MS 11, ni mkulima wa shamba lenye ukubwa wa ekari 2 na mfugaji wa ng'ombe 3.


ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu mara nyingi huwashauri wakulima wenzie kulima kwa wakati na kupanda mbegu bora na kwa kipimo, kutumia mbolea na kunyunyizia dawa pindi wadudu wanapoharibu mazao. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 20"
MARTINA GEORGE CHITETE (32) mkazi wa Mufindi Iringa nambari yake ya ushiriki ni MS 06, yeye ni mkulima na anashamba lenye ekari 2.

ANADHANI YEYE NI MFANO WA KUIGWA: Kwa sababu wana utaratibu wa ujenzi wa shule  pamoja shughuli zingine ambazo huratibiwa na uongozi wa kijiji. "Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 2. Kwa mwaka ninavuna mazao gunia 14"


Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na kusimamiwa na Oxfam limefikia tamati ya hatua ya awali ya kutafuta washindi kwa kutangaza wanawake 20 kuingia katika top 20 ya shindano hilo la aina yake.

Wanawake hao wenye wasifu tofauti tofauti sasa wataingia katika kijiji cha maisha plus kwa muda wa wiki tatu ikiwa ni katika hatua ya kutafuta mshindi wa shindano hilo ambalo linalenga kuhamasisha jamii juu ya kilimo, hifadhi ya chakula na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na njaa. Mbali na wanawake hao 20 pia kuna mshiriki mmoja ambaye yeye amepatikana kwa shindano la mtandaoni.

Hapa nakuletea orodha ya akina mama hao mmoja baada ya mwingine. 


Na tabianchi blog