Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kigoma jana jioni akitokea Rwanda, tayari kuendelea na ziara ya siku
tano katika Mkoa wa Kigoma, kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama na
kukagua miradi ya maendeleo inayoyekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
Kinana
akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Walidi Kaburu baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma.Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM kutoka Zanzibar, Ally Karume.
Gwaride la Vijana wa CCM, likiwa tayari wakati wa mapokezi hayo ya Kinana.
Kinana akivishwa skavu na kijana Hadja Kanyoe wakati wa mapokezi
Vijana wa CCM wakimpigia makofi Kinana uwanjani hapo
Kinana
akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
aliyfika kumlaki uwanjani hapo na kuungana naye kwenye ziara ya mkoa huo
na wa Katavi.Nape alikuwa Chalinze ambako alikuwa Mratibu Mkuu wa
Kampeni za Uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Chalinze ambapo
Ridhiwani Kikwete wa CCM ameibuka mshind na kuvibwaga kwa mbali vyama
vingine vya upinzani.
Kinana
akisalimiana na Ofisa wa CCM ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa
magazeti ya chama ya Uhuru na Mazalendo, Bashir Nkoromo. Nkoromo pia
anaiendesha Blog ya CCM.
Kinana
akiwa na viongozi wa CCM Mkoa wa Kigoma pamoja na Mkuu wa Mkoa huo,
Kanali mstaafu Issa Machibya waliofika kumlaki uwanjani hapo.
Nape
akielezea jinsi CCM ilivyoshinda kwa kishindo katika chaguzi za
Chalinze, Kalenga na madiwani wakati wa mkutano wa Halmashauri ya Mkoa
wa Kigoma
Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma wakisikiliza kwa makini wakati
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza nao leo baada ya kupewa taarifa
ya mkoa huo.
Kinana
akizungmza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma
kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Kigoma jana.
Nape akigalia mawe yanayotumika kujengea mabanda ya maduka yanayojengwa na CCM Mkoa wa Kigoma
Kinana akikagua ujenzi wa mabanda ya maduka mradi wa CCM Mkoa wa Kigoma
Kinana
akiongozwa na Mchumi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Kadri Mushi kukagua mabanda
ya maduka yanayojengwa na CCM Mkoa wa Kigoma.
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA
MATUKIO BLOG