Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya 15 bora wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kuchaguliwa washiriki watano bora.
Hawa ndio washiriki walioingia tano bora
Emiliana
Fidelis akiwa amesimama mbele ya meza ya majaji mara baada ya majaji
kufurahishwa na kuvutiwa na Kipaji chake, Emiliana ni mmoja kati ya
waliotakiwa kuwa mshindi wa Kanda ya ziwa ila kwa bahati mbaya Umri wake
ndio ulikuwa kikwazo.
Jaji
Yvonne Cherry akimkabidhi zawadi ya shilingi laki Moja Mshiriki Emiliana
Fidelis mara baada ya kuvutiwa na Kipaji chake huku akiwa mshiriki
pekee mwenye umri mdogo kuliko wote kwenye mashindano ya Kusaka Vipaji
vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents.
Jaji
Mkuu wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania yajulikanayo
kama Tanzania Movie Talents, Roy Sarungi akimkabidhi zawadi mmoja wa
Washindi watatu wa mashindano hayo mara baada ya kutangazwa washindi.
Jaji Single Mtambalike akimpongeza mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuibuka kidedea katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents.
Mshiriki
Crensenciah Herman akilia kwa furaha mara baada ya Kutajwa kuwa mmoja
kati ya washindi katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lilomalizika Leo Mkoani Mwanza
Majaji
wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi watatu wa Kanda ya Ziwa
Mkoani Mwanza mara baada ya Kuwatangaza na kuwakabidhi washindi zawadi
zao.
Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza