Kulia
ni mwili wa marehemu baada ya kuchomwa moto-kushoto ni Machela
ikiandaliwa kuupakia mwili wa kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto |
Kijana aliyejulikana kwa jina la Mangi akiwa ndani ya gari, pembeni yake ni maiti ya mwenzake |
Polisi wakikagua makoti ambayo kijana aliyenusurika alikuwa ameyavaa |
Mtu
mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina
anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha
kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa.
Tukio
hilo limetokea jana alfajiri katika kijiji cha Shibula kata ya
Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea
usiku wa kuamkia jana katika mtaa wa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki
moja na paneli ya solar ziliibiwa.
Katibu
wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa
kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji
vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana
mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai
wanatafuta pikipiki iliyopotea.
Mashalia
ameongeza kuwa kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa
mara ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.
Kwa
upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka
wananchi wa kata hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba
wawasiliane na uongozi wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo
CRD: malunde blog..