SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, March 29, 2014

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR AFUNGA MAFUNZO YA SIKU TATU JUU YA VIKWAZO VYA BIASHARA VISIVYO VYA KIUSHURU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum akifunga mafunzo ya siku tatu kwa washiriki juu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa TradeMark Afrika Mashariki kupitia Tanzania Asaac Mtwale akiwashukuru washiriki wa mafunzo juu ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru bara maada ya kufungwa kwa mafunzo hayo katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum (hayupo pichan) alipokua akifunga mafunzo hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum (wakatikati waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya vikwazo vya Biashara visivyo vya kiushuru yaliyofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar. 
 (PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR).