Muonekano wa ukumbi wa bunge ambako Wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba mjini Dodoma ambamo Wajumbe wanakutana kujadili rasimu ya kanuni
za Bunge Maalum za mwaka 2014 leo.Picha na Muhidin Issa Michuzi
====******====
Picha Mbalimbali Kutoka Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Jenista Mhagama (Kushoto) ambaye pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Bi. Christowaja Mtinda
wakiwasili katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya Semina ya uundwaji wa
kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa bunge
maalum la Katiba Jumanne Maghembe ambaye pia ni Waziri wa Maji akiwa na
Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo wakiwasili katika ukumbi wa Bunge kwa
ajili ya Semina ya uundwaji wa kanuni za kuongoza Bunge Maalum la Katiba
leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Vuai ally Vuai akiongea leo katika semina
ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba
na kuwataka wajumbe kufuata yale aliyoyasema Waziri Mkuu ya kuzingatia
Staha ya Lugha katika Vikao vya Bunge Maalum la katiba leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi(Kushoto) leo mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo Wajumbe wa Bunge
hilo leo Mjini Dodoma
Baadhi ya wa Bunge Maalum la Katiba waliohudhuria katika semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Samweli Sitta akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge hilo
ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven
Wassira( Kulia). Leo Mjini Dodoma. Chini yao ni wajumbe wa Bunge Hilo
Seif Khatibu( Kushoto) na Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiongea na
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na kuwataka kuzingatia maadili na
lugha fasaha katika kikao hichi ili kufikia lengo linalotazamiwa kwa
maslahi ya Taifa.Wakati wa semina ya kuunda kanuni zitakazotumika katika
vikao vya Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Picha na Hassan Silayo-Maelezo
0 comments:
Post a Comment