SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, March 30, 2014

MASHALI AMGALAGAZA KASEBA KWA POINTI

 Bondia Thomas Mashali (kushoto) akikwepa konde la Japhet Kaseba, wakati wa pambano lao kuwania Ubingwa wa WBO uliofanyika kwenye ukumbi wa UBO Africa Mashali.  Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Mashali alimshinda mpinzani wake kwa Pointi.
 
 Japhet Kaseba (kushoto) akiwa na mpinzani wake, Jamhuri Kaseba,
Mashali, akipozi na mikanda yake baada ya kukabidhiwa mkanda mmoja usiku huu.
Mabondia Japhert Kaseba (Thomas Mashali) wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali. Mashali alishinda kwa Pointi
KWA MATUKIO ZAIDI YA PAMBANO HILI NA YA UTANGULIZI PAMOJA NA VIDEO YA PAMBANO LA KASEBA NA MASHALI, ZITAKUJIA BAADAYE.


=======================================

WBO WATOA UJUMBE MASHALI AKIMGALAGAZA KASEBA KWA POINT
Mabondia Japhert Kaseba na Thomas Mashali wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali alishinda kwa Pointi.
Mtoto Zainabi 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa katika kona ya bondia Japhert Kaseba kabla ya kuanza kwa mpambano wao mkanda uho aliubeba kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki pamoja na mabondia waliokuwa wakiwania mkanda huo

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa kabla ya mpambano kuanza katika kona ya Thomas Mashali ambaye alishinda na kuunyakuwa mkanda huo kwa kushinda kwa point.

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo uku Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa akiwakumbusha mabondia Thomas Mashali kushoto na Japhert Kaseba sheria zitakazotumika katika mpambano huo.
Bondia Kalage Suba kushoto akipambana na Alan Kamote wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO katika ukumbi wa PTA Sabasaba Kamote alishinda kwa TKO ya raundi ya saba.

Bondia Alan Kamote akiwa na ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo
Baadhi ya watoto ambao wanafanya mazoezi katika GYM mbalimbali walijitokeza kuamasisha ujumbe wa World Boxing Ordanization 'WBO'  kushoto nio Rashidi Matumla na kulia ni Promota kutoka tanga Ally Mwazoa ambaye anakuja kwa kasi uku akiwa na mapasmbano matatu mfululizo yatakayofanyika PTA Sabasaba

Mabondia wakongwe Jock Hamisi kushoto akipambana na Said Chaku wakati wa mpambano wao waliotoa droo

Katika kuhakikisha ujumbe wa WBO unazingatia mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akipiga padi huku akisimamiwa na Emanuel Mlundwa

Baadhi ya watoto waliojitokeza katika kampeni ya kufanya mazoezi watoto wasipewe madawa wakiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali uku wakiwa na zawadi zao walizopewa mabegi flana na glove zenye ubora wa ali ya juu

Zainabu 'Ikota' Mhamila