KOCHA David Moyes ameimaliza vizuri wiki yake ngumu baada ya kushinda mabao 4-1 dhidi ya Aston Villa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Mabao mawili yaliyofungwa na Wayne Rooney dakika za 20 na 45 kwa penalti na mengine ya Juan Mata dakika ya 57 na Javier Hernandez dakika ya 90 yalitosha kuiongezea pointi tatu muhimu Man United.
Villa ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ashley Westwood dakika ya 13 kwa mpira wa adhabu.
United sasa inatimiza pointi54 baada ya kucheza mechi 32 na inaendelea kubaki nafasi ya saba nyuma ya Tottenham Hotspur yenye pointi 56 za mechi 31.
Ndege iliyoandaliwa na baadhi ya mashabiki wa Manchester na kuipitisha juu ya paa la Old Trafford haikuwa na madhara yoyote kwa kikosi cha Moyes na kumfanya awe na furaha.
Kikundi cha mashabiki wa Man United kilikodi ndege kwa Euro 840 na kuirusha juu ya paa la Old Trafford.
Ujumbe ulioandika kwenye ndege hiyo ulikuwa unamhusu David Moyes uliosomeka ’Wrong One – Moyes Out’, kwa tafsiri ya “Mtu ambaye si sahihi. Moyes nje”
Lakini kama mashabiki walikusudia kumzodoa Moyes, basi walichemka kwani mashabiki wengi leo walimuunga mkono kocha huyo.
Mashabiki wa nyumbani wa Man United waliizomea ndege iliyokuwa ikizunguka Old Trafford na nyimbo za kumsifu Moyes zilisikika mara kwa mara.
Jembe: Wayne Rooney alifunga mawili katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya beat Aston Villa
Furaha: David Moyes aliwanyanyua mashabiki wa Man United nyumbani Old Trafford baada ya kupata ushindi dhidi ya Aston Villa
Kikosi cha Manchester United: De Gea 6, Rafael 5.5 (Carrick, 45), Jones 6.5, Vidic 6.5, Buttner 6; Fletcher 7, Fellaini 6; Kagawa 7.5 (Januzaj, 67), Mata 7.5, Young 5.5; Rooney 8 (Hernandez, 74).
Kikosi cha Aston Villa: Guzan 6; Bacuna 5, Clark 6, Vlaar 5.5, Bertrand 6; Westwood 7, Delph 5.5, Albrighton 6.5 (Lowton, 78); Weimann 5, Benteke 5.5, Agbonlahor 5 (Tonev, 71)
Mwanzo mzuri: Ashley Westwood aliifungia Aston Villa bao la kuongoza katika dakika ya 13
Ashley Westwood alifunga bao kwa kupiga shuti lililopita ukuta wa Man United na kumwacha De Gea hana la kufanya