Moshi Hussein ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi nyumbani kwa baba
yake mzazi huko katika kijiji cha Magiri wilaya ya Uyui mkoani
Tabora,binti huyu ana umri wa miaka 13 hajawahi kupelekwa Shule kwa
maana ya kupata haki kama wapatavyo watoto wengine,Moshi amekuwa
akililia hilo kwa baba yake mzazi bila mafanikio.Jambo baya zaidi kwa
mujibu wa maelezo ya Moshi baba yake anahitaji aolewe ili aweze kupata
Ng'ombe licha ya kuwa ana umri mdogo na hawezi kukabiliana na Changamoto
za ndoa kulingana na ulemavu alionao.
Moshi kwakuwa hana uwezo wa kutembea umbali hata wa hatua kumi anawaomba
wasamalia wema kumsaidia mambo makubwa matatu,kwanza ikibidi kumuondoa
nyumbani kwao ili aepukane na ndoa ya lazima,Pili apelekwe shuleni
kwakuwa anaona kukaa kwa baba yake ni wazi kwamba atakuwa anatafuta
umasikini mwingine wa ziada ukiachana huo wa ulemavu wa viungo ambao
umekuwa kikwazo kikubwa hata cha kujihudumia masuala mengine ya kiutu wa
mwanamke.Kwa mujibu wa maelezo yake Moshi ana mshangaa baba yake kwa
uamuzi wa kutaka aolewe kwakuwa hata ndoa yenyewe haoni kama itakuwa na
maana kutokana na ulemavu alionao na pia haoni sababu ya kuwa mzigo kwa
mtu mwingine katika maisha yake.
Moshi amekuwa akijikatia tamaa kulingana na ulemavu alionao,"Kama
ningekuwa na mama labda hata ningeweza kupelekwa shule na mimi ningekuwa
msomi kama wengine,lakini kwa hali hii ni bora hata ningekufa nimfuate
mama yangu huko aliko"
Via KapipiJHabari
0 comments:
Post a Comment