Muigizaji
msaidizi katika Filamu ya 12 Years, Lupita Nyong'o akionyesha wazi
hisia zake baada ya kushinda tuzo hiyo kwa muigizaji msaidizi bora
zaidi. Alicheza kama msichana mtumwa ambaye alipendwa na bwenyenye wake.
Lupita
Nyong'o:Nyota wa filamu '12 Years a Slave' alikuwa muigizaji msaidizi na
baada ya kuteuliwa kwa tuzo hiyo, alifanikiwa kuinyakua katika hafla ya
tuzo za Oscars
Kama
ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita
Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa
jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya
''12 Years A Slave.''Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema "
Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha
yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''Kisha Lupita
akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote
unakotoka, ndoto zako ni halisi.''Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo
la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha
ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV
katika filamu Dallas Buyers Club.Alilazimika kupunguza uzani kwa
kipindi kifupi ili kuigiza.Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika
mjini Los Angeles nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment