Bango linalo onesha warsha ya kwanza ya Wadau wa Mfuko wa Misitu Tanzania
Mfuko
wa Misitu Tanzania ni Mfuko wa hifadhi ambao umeanzishwa kisheria kama
njia endelevu ya kuwezesha uhifadhi wa rasilimali za misitu hapa
nchini.Mfuko huu umeanzishwa kwa lengo la kukabiliana na changamoto za
usimamizi wa rasilimali za misitu hasa katika kuimarisha utekelezaji wa
Sera na Sheria ya Misitu.
Mfuko
ilianza kazi rasmi Julai 2011.Mfuko wa Misitu Tanzania ni wa Umma na
unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini.Katika utendaji wa kila siku,Bodi ya
Wadhamini inasaidiwa na Sekretarieti.
Mfuko
wa Misitu Tanzania unafanya shughuli zake maeneo yote ya Tanzania Bara
ambapo hutoa ruzuku kwa wadau wote wanojihusisha na usimamizi wa
rasilimali za misitu na uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi waishio
pembezoni wa misitu
Wadau wa Mfuko
Wadau
wa Mfuko wa Misitu Tanzania ni kama ilivyoanishwa katia muongozo wa
uendeshaji Mfuko ni pamoja na jamii;Asasi za jamii;watafiti na Taasisi
za Utafiti; wanamazingira;Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania;Tasisi za
mafunzo ya misitu na nyuki;Wizara ya Maliasili na Utalii;Serikali za
Mitaa zikiwemo Halimashauli za Wilaya;Taasisi zisizo za kiserikali (
NGOs) na Asasi za kiraia.
Dhumuni la warsha hii lilikuwani kujadiliana na wadau kuhusiana na mambo ya fuatayo
Dira
Kuwa
chanzo cha muda mrefu na endelevu cha fedha za kughalamia usimamizi wa
rasilimali misitu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Dhamira
Mfuko
unahakikisha upatikanaji endelevu wa fedha za kugharamia usimamizi wa
rasilimali misitu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Pia kuelewesha wadau na kujudiliana nao dhumuni na majukumu ya Mfuko kama ifutavyo:
Madhumuni ya Mfuko kama yalioanishwa katika kifungu cha 80 cha Misitu Sura ya 323 ya mwaka 2002.
Majukumu ya Mfuko
(i) kuhamasisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko.
(ii)
kutoa ruzuku kwa wadau wa misitu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
uhifadhi na uendelezaji wa misitu katika maeneo ya usimamizi yaliopo nje
ya maeneo ya wakala wa Huduma za Misitu Tanzana.
(iii) Kutangaza Mfuko kwa lengo la kupata wafadhili.
(iv) Kuhakikisha shughuli za Mfuko na miradi iliyofadhiliwa na Mfuko inatekelezwa kulingana na kanuni na miongozo.
(v) Kujenga uwezo wa watendaji wa Mfuko juu ya usimamizi wa rasilimali za misitu na za Mfuko
Warsha pia inajadili jinsi gani ya kuutangaza Mfuko ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na Wadau wa Mfuko
Changamoto zinazokabili Mfuko wa Misitu Tanzania.
Kuwezesha
miradi zaidi a 200 kwa kipindi cha miaka mitatu bado Mfuko unakabiliwa
na uhaba wa fedha kulingana na matarajio a wadau.Kwa sasa chanzo cha
mapato ya Mfuko ni serikali kutoka kwenye vyanzo vilivyoainishwa kwenye
sheria ya misitu ya mwaka 2002 .Hivyo mikakati ya muda mfupi na a muda
mrefu inahitajia kwa ajili ya kutafuta vyanzo zaidi vya mapato nje ya
serikali.Mfuko wa misitu Tanzania umeanza mchakato wa kuandaa mkakati wa
kutafuta vyanzo zaidi vya fedha ili kuboresha mapato yake
Wadau
watajadili Changamoto zinazokabili Mfuko wa Misitu Tanzania na nini
kifanyike kupunguza changamoto hizo kama si kuziondoa kabisa
,Sekretarieti wakiwa katika mikakati ya kuhakikisha mkutano huu
unakwenda sawasawa
0 comments:
Post a Comment