Aziza Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.
Aziza Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.
Nyumba ambayo familia ya Aziza Maohamed ilikuwa ikiishi awali kabla ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua katika kitongoji cha Kijweni kijiji cha Mijongweni kata ya Machame/Weruweru.
Sehemu ambayo analala kwa sasa mtoto wa Aziza Mahamed,Sikujua Aloyce.
Nyumba ya familia ya Aziza Mohamed iliyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita wilayani Hai.
Misaada toka Bonite bottlers ikishishwa
Mabati yakishushwa kijijni hapo
Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa bati na chakula kwa mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga kwa ajili ya wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo iliyoezua paa za nyumba huku kaya zaidi ya 1000 zikikosa makazi na chakula
Mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa bati na chakula kwa mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga kwa ajili ya wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo iliyoezua paa za nyumba huku kaya zaidi ya 1000 zikikosa makazi na chakula
Choo hicho kinavyoonekana kwa nje.
Baadhi ya majengo yaliyoezuliwa na upepo katika kitongoji cha Kijiweni wilayani Hai.
Hali mbaya
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akiteta jambo na katibu wa mbunge wa jimbo la Hai,Richard Mtui.Kulia kwa ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai,Merikizedeck Humbe.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.
FAMILIA moja ya watu watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka saba
imelazimika kuhamishia makazi chooni baada ya paa la nyumba waliyokuwa
wakiishi kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha
wiki iliyopita katika wilaya ya Hai.
Familia hiyo ya Aziza Mohamed (55) mwanae wa kiume, Sikujua Aloyce
(40) na mjukuu wake wakazi wa kitongoji cha Kijiweni kijiji cha
Mijongweni kata ya Machame Weruweru imekuwa ikiishi kwa zaidi ya siku
14 katika choo hicho ambacho paa lake lilisalimika wakati mvua hiyo
ikinyesha.
Akizungumzia tukio hilo Aziza alisema wakati mvua hiyo iliyoambatana
na upepo mkali ikinyesha alikuwa ametoka nyumbani kwake na kwamba
baada ya kuona hali imekuwa mbaya akalazimika kukimbia kurudi
nyumbani.
"Mvua ilivyokuja nilikuwa sipo nilivyoona hali imekuwa ni mbaya na
upepo uliokuwepo ikabidi nikimbilie nyumbani ,nikaanza kumtafuta huyu
mtoto na baba yake,nikawa na tangatanga nataka nipike sasa vile
nashangaa shangaa kutaka kujua mtoto yuko wapi nikaona kidogo nyumba
inafunuliwa bati nikiwa humo humo ndani."alisema Aziza.
"Kumbe mtoto na baba yake walikuwa wako chumba cha pili Nyumba kubwa
ndipo baadae nikamsikia mtoto ikabidi nianze kupiga kelele tokeni huko
tokeni huko,ndio wakatoka ikabidi tukimbilie huku chooni tukaja
kupumzika mpaka mvua ikaisha ambako tunaishi hadi sasa."aliongeza
Aziza.
Alisema hivi sasa choo hicho wamekuwa wakikitumia nyakati za mchana
kwa ajili ya kujisaidia na kwamba ifikapo usiku hulazimika kufunika
shimo la choo hicho kwa gunia ,na kisha kuweka matandiko kwa ajili ya
kulala.
Mengi,Mbowe watoa msaada wa chakula na bati.
Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi kupitia kampuni
tanzu ya Bonite Bottlers ya mjini Moshi ametoa msaada wa mabati
200,kilogramu 2500 za unga pamoja na kilogaramu 100 za maharage kwa
ajili ya kusaidia familia zilizo athirika na mvua hizo.
Akikabidhi msaada huo juzi mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa
kampuni ya Bonite Bottlers Christopher Loiruk alisema Mwenyekiti wa
makampuni ya IPP,Mengi pamoja na uongozi wa kiwanda umeguswa na
tatizo hilo kwa kuona kuwa walioathirika ni watanzania wenzetuhivyo
hawana budi kupatiwa msaada.
"Kama Bonite Bottlers na Mwenyekiti wetu ,Reginald Mengi tumeguswa na
tatizo hili kwa kuona kuwa hawa ni Watanzania wenzetu,wana Kilimanjaro
wenzetu,ndugu zeti na tunafahamu matatizo hayapigi hodi, kwa hiyo
yanapotokea ni lazima sote tuoneshe uzaledo ili tuweze
kusaidiana"alisema Loiruk.
"Tumeanza kwa kutoa mabati 200,tuna vyakula unga kilo 2500,na maharage
kilo 100 tunaomba muwakilishe kwa waathirika ,tunaomba makampuni
mengine na hata watu binafsi waweze kuja kuwasaidia hawa watu ambao
hawana mahala pa kukaa na hata chakula."aliongeza Loiruk.
Kwa upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Hai,Richard Mtui alisema
Mbunge wa jimbo la Hai ,Freeman Mbowe tayari amekabidhi bati 26 kwa
familia zilizofikwa na tatizo hilo huku akiahidi kutoa kiasi cha sh
milioni 7 ambapo sehemu ya fedha hizo zinatoka katika mfuko wa jimbo
wa Mbunge .
CHANZO: MICHUZI MATUKIO BLOG
0 comments:
Post a Comment