Taarifa za kifo cha mwigizaji nguli wa Marekani Will Smith zilisambaa kama moto nyikani mapema wiki hii, na kusababisha mtafaruku kwa mashabiki wake duniani kote. Hata hivyo taarifa ya jana Ijumaa February 21, 2014 zimethibitisha kuwa habari hizo za uzushi na uwongo ni mojawapo ya nyingi zinazohusisha watu maarufu.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa na Globu ya Jamii, ukweli ni kwamba mwigizaji huyo aliyetamba katika filamu kadhaa ziiwemo The Pursuit of Happyness, Men in Black orThe Fresh Prince of Bel-Air bado anadunda.
Uzushi wa kifo cha Will Smith unasemekana ulianzia kwenye ukursa mmoja katika mtandao wa jamii wa Facebook siku ya Alhamisi uliokuwa na kichwa cha habari ‘R.I.P. Will Smith’ n kuvutia wasomaji takriban milioni moja.
Waliosoma ukurasa huo walishawishika kuamini taari hiyo iliyosomeka:
“Mnamo majira ya saa 11 a.m. ET siku ya Alhamisi (February 20, 2014), mwigizaji wetu kipenzi Will Smith alitangulia mbele ya haki. Will Smith alizaliwa September 25, 1968 huko Philadelphia. Tutamkosa lakini hatutomsahau. Tafadhali onesha kuguswa kwako kwa ku ‘like’ ukurasa huu.
Ghafla tu mamia ya mashabiki wakaanza mara moja kuandika ujumbe wa rambirambi kwenye ukurasa huo wa Faceboook, wakionesha kusikitishwa kwao kwa kifo cha muigizaji na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 45.
Kwenye twitter nako taarifa hiyo ilivuma balaa.
Wakati baadhi ya mashabiki waliiamini taarifa hiyo, wengine waliguna na kujiuliza mara mbilimbili bila shaka wakichukulia uzoefu wa taarifa feki za aina hiyo zilizopata kutokea miezi ya karibuni. Wengine pia waliuliza iweje habari ya kifo cha mtu kama Will Smith isitangazwe kwenye vyombo vikubwa vya habari.
Utafiti pia ukaonesha kuwa asilimia 80 ya waliohojiwa kuhusu uzushi wa kifo cha Will Smith sio za kufurahisha kidogo.
Ndipo Ijumaa hii (Februari 21) wawakilishi wa Will Smith walithibitisha kuwa hajafa.
“Anajiunga katika orodha ndefu ya watu maarufu walioathirika na uzushi kama huo. Yeye bado yu hai na buheri wa afya, acha kuamini unachokiona mitandaoni”, walisema.
Baadhi ya mashabiki walielezea hasira zao kwa taarifa hiyo feki, wakisema ni ya kuhamanisha na kujeruhi hisia zao. Wengine walisema taarifa hiyo inaonesha ni jinsi gani Will Smith anavyojulikana ulimwenguni kote, ikiwemo Tanzania ambako nako taarifa za kifo hicho feki zimezagaa kwenye mitandao ya jamii.
Hivi tunavyoongea kituo maarufu cha TV cha Home Box Office
(HBO) iko katika hatua za mwisho kuandaa onesho la kuchekesha litalomhusisha
Will Smith (kulia) pamoja na mwanamuziki mahiri Jay Z (wa pili toka kulia). Wawili hawa (wanaoonekana pichani na wake zao Beyonce na Jada Pinckett-Smith) pia kwa pamoja
wanatengeneza filamu iitwayo ‘Annie’ inayotegemewa kuzinduliwa mwezi Desemba
mwaka huu. Vile vile kampuni ya Will Smith ya Overbrook Entertainment imeungana
na kampuni ya Jay Z Roc Nation kuandaa filamu ya ‘Free Angela & All
Political Prisoners’.
Will Smith na mkewe Jada Pinckett-Smith walizuru Tanzania mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka 2008, na kutembelea Zanzibar na Arusha, wakati huo akiwa kama Balozi wa Hisani wa kupambana na malaria duniani. Globu ya Jamii ilirekodi ujio huo kama picha zinavyoonesha hapa chini.
Will Smith akiongea na Rais wa Zanzibar wakati huo (Agosti 30, 2008) Dkt Amani Abeid Karume alipomtembelea Ikulu, Zanzibar katika ziara yake ya Tanzania akiwa kama Balozi wa Hisani wa kupambana na Malaria duniani
Will Smith akimpa zawadi ya kitabu Dkt Karume
Will Smith na mkewe Jada Pinckett-Smith wakipozi na Dkt Karume na Mama Shadya Karume Ikulu, Zanzibar
Will Smith na mkewe wakiwasili hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam Siku ya Jumanne ya Agosti 26, 2008
Will Smith na mkewe pamoja na mlinzi wao wakifurahia kamera ya Globu ya Jamii mara baada ya kuwasili Kilimanjaro hotel
Mhudumu wa hoteli ya Kilimanjaro akiwapokea Will Smith na mkewe pamoja na mlinzi wao
Will Smith akiwa na Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza Vyandarua cha A to Z jijini Arusha, Bw. Anuj Shah, alipotembelea siku ya Jumatatu ya Septemba 1, 2008
NA ANKAL MICHUZI
NA ANKAL MICHUZI
0 comments:
Post a Comment