Ndege iliyotekwa ikiwa imetua nchini Uswisi. Picha ya Maktaba
Msaidizi wa rubani wa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Halimedhin
Abera, ndiye aliyebainika kuteka moja ya ndege za shirika hilo hivi
karibuni.
Inadaiwa kuwa rubani huyo aliiteka ndege kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo, baada ya kufiwa na mjomba wake.
Abiria mmoja aliyenusurika katika ajali hiyo anasema, Abera aliwaamuru
abiria wote kukaa chini, huku akiwatishia kuzima hewa ya Oksijeni.
Abera, ambaye amelifanyia kazi shirika hilo kwa miaka mitano, inadaiwa
alifunga mlango wa chumba cha rubani (cockpit) na kubadilisha mwelekeo
wa ndege. Awali ndege hiyo ilikuwa ikielekea Italia, lakini akaamua
kuipeleka Uswisi aliposema alikwenda kuomba hifadhi. Msimuliaji huyu wa
mkasa anasema baada ya kuiteka ndege alifungua maski za hewa ya
oksijeni na kutishia kuizima kama abiria wasingetulia.
Anasimulia: “Nilifikiri labda kuna tatizo la kiufundi au kwa bahati
mbaya mtu amebonyeza sehemu, abiria tulibaki tukitazamana kwa sura za
kuulizana ndani ya ndege.”
Anasema baada ya muda mfupi, sauti nzito ikizungumza kwa jazba
ilisikika kutoka katika vipaza sauti vya ndege ikisema: “Kaa chini,
ninazima hewa ya oksijeni”.
Msimuliaji anasema rubani huyo alikaa kimya kwa saa sita bila
kuzungumza, huku abiria wakiwa hawajui wanaelekea wapi wala mwisho wao
utakuwa vipi.
Anaongeza kusema kuwa wakati hayo yanaendelea, wahudumu wa ndege
waliendelea kugawa vinywaji, huku wakiwatuliza abiria na kuwahakikishia
kuwa safari ilikuwa salama.
Hata hivyo, wahudumu hao waliwaambia kuwa, hawana mawasiliano na rubani huyo kwa kuwa ameyakata.
“Wahudumu walikuwa wanagawa vinywaji na kutoa maneno ya faraja, hata
hivyo kuna wengine walikuwa wakitokwa machozi mbele yetu,” anasema
msimuliaji.
Baada ya kusafiri saa sita kimyakimya, ghafla ndege ilianza kuzunguka
huku ikiegemea upande mmoja na baada ya muda ilibadilisha upande wa bawa
jingine.
Anasema: “Niliona mwisho wetu umefika kwani ndege sasa inaanguka.
Nikitazama nje niliona mwanga lakini baada ya dakika mbili nikaona giza
tena,” anasema na kuongeza:
MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment