Rais Jakaya Kikwete
akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dk. Charles Kimei, (kushoto), alipofika kutoa msaada wa sh. milioni 100 kwa ajili ya kusaidia waathirika
wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo
katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita. Dk. Kimei alifuatana na baadhi
ya viongozi wa benki hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto),
akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei.
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma
kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.ikulu jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bernki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), Naibu
Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka na Mkurugenzi
wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), ikulu
jijini Dar es Salaam.,
Dk. Kimei akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete.
Mazungumzo yakiendelea.
Dk.
Charles Kimei akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi hundi ya Sh,
milioni 100 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea mkoani
Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete
akipokea hundi ya sh. milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), kwa ajili ya kusaidia watu waliopatwa na
mafuriko Mkoani Mororo hivi karibuni.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia kwa makini hundi aliyokabidhiwa.
Rais
Jakaya Kikwete akiiweka katika bahasha hundi ya Sh, milioni 100 baada ya
kupokea kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei (kushoto), huku makini hundi aliyokabidhiwa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka
Rais Dk. Jakaya Kikwete akimkabidhi hundi aliyokabidhiwa na uongozi wa Benki ya CRDB kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi anayeshughulikia pia masuala ya maafa, William Lukuvi.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Njia Mbadala za Kibenki katika Benki ya CRDB, Joseph Witts.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia), akiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Benki ya CRDB, John Lugambo.
Rais
Dk. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya
CRDB, Kushoto ni Katibu wa Benki ya CRDB, John Lugambo, Mkurugenzi
wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka, Mkurugenzi wa Idara ya Njia Mbadala za Kibenki,
Joseph Witts na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu.
Rais
Jakaya Kikwete (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Benki ya CRDB mara baada ya kupokea hundi ya sh. milioni 100 kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili
kushoto), kwa ajili ya kusaidia watu waliopatwa na mafuriko Mkoani
Mororo hivi karibuni. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (wa pili kulia), na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Rais
Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dkt. Charles Kimei, baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni
100 kutoka benki hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyozikumba
wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Februari 4, 2014, amepokea hundi ya Sh. milioni 100 kutoka Benki ya CRDB kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita.
Rais Kikwete amekabidhiwa hundi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, na kuhudhuriwa pia na Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia pia masuala ya maafa.
Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi hiyo kwa Rais Kikwete, Dkt. Kimei amesema kuwa fedha hizo ni sehemu ya Sh. Milioni 850 ambayo ni asilimia moja ya faida ya Benki hiyo ambayo hutengwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za jamii.
“Sote tumeona madhara makubwa yaliyosababishwa na mafuriko haya. Watu wengine wamepata hasara – akinamama, watoto, wajawazito na wazee. Hawa wote wanahitaji misaada ya ziada ili kukabiliana na athari za mafuriko hayo,” amesema Dkt. Kimei.
Akizungumza kabla ya kupokea hundi hiyo, Rais Kikwete ameelezea kwa ufupi mafuriko hayo yaliyotokea alfajiri ya Januari 22, mwaka huu, 2014 na athari ambazo zimetokana na mafuriko hiyo katika maeneo ya Magole, Dakawa na Mateteni huko Dumila, Wilaya ya Mvomero, ambayo aliyatembelea mwishoni mwa mwezi uliopita kujionea madhara.
“Waswahili husema kuwa ajali haina kinga na ni kweli. Unajua mafuriko yaliyotokea katika eneo la Dumila hayakutokana na wala na mvua ya pale. Mvua ilinyesha kule Kiteto, Mkoa wa Manyara, lakini walioathirika kwa mafuriko ni hawa jamaa zetu wa Dumila. Bahati tu ni kwamba mafuriko hayo yalilikumba eneo hilo alfajiri wakati watu tayari wameamka na ndio maana hakuna mtu aliyepoteza maisha yake katika eneo hilo,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Watu wamepata hasara kubwa. Baadhi nyumba zao zimesombwa na kuzolewa na maji, nyingine zimebomoka, watu wamepoteza mali zao nyingi kama vile nguo na wengine hata chakula chao kimesombwa na maji. Wanahitaji msaada na kwa kweli sisi katika Serikali tunaishukuru sana CRDB kwa kutoa msaada huu kwa sabababu unachangia katika jitihada za Serikali kukabiliana na tatizo hili.”
Akizungumza katika shughuli hiyo, Mheshimiwa Lukuvi amesema kuwa tathmini mpya imeonyesha kuwa watu walioathirika katika mafuriko hayo ni 9,268 na kati ya watu hao kaya 522 hazina makazi kabisa baada ya nyumba zao kubomolewa na maji, nyingi zaidi 466, zikiwa katika Wilaya ya Kilosa.
Amesema kuwa nyumba 537 zimeharibika hata kama wenye nyumba hizo bado wanaendelea kuishi ndani ya nyumba hizo na nyingine 1,036 ziliingiwa na maji hata kama hazikuharibika.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
04 Februari, 2014
0 comments:
Post a Comment