Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yahya Khamis Hamad,
akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo alipowasili katika Ofisi ya Katibu wa Baraza kwa ajili
kujitambulisha na kuhudhuria kuapishwa kwake kuingia katika Baraza la
Wawakilishi baada ya kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo
la Kiembesamaki uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho
akiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuaza kwa
taratibu za shughuli za Kikao na kumapisha Mwakilishi Mpya wa Jimbo la
Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. wakati wa Kikao cha
asubuhi leo.
Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho akisoma Dua kabla ya kuanza kwa Kikao cha Baraza cha Asubuhi leo.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wanawake wakimshindikiza
Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiingia
katika ukumbi wa Mkutano tayari kwa kuapishwa kwake kuwa Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar baada ya
kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa
wiki.
Mhe Mhmoud Thaib Kombo, akiapishwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi
kuwa Mwakilishi wa Jimbola Kiembesamaki, baada ya kushinda Jimbo hilo na
kuwa Mwakilishi Mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa mwakilishi wa jimbo
hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitia saini baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Kiembesaki Zanzibar kwa kupata
ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Mapinduzi Pandu Ameir Kificho akimkabidhi
Vitendea Kazi vya Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la
Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.baada ya kuapishwa kuwa
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Waheshimiwa Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mwakilishi
wao wa Jimbo la Kiembesamaki wakati akiapishwa katika ukumbi wa
Mkutanona Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho leo
asubuhi.
Wanafamilia ya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakihudhuria sherehe za
kuapishwa kwake leo asubuhi katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wageni walioongozana na Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakisimama wakati wa
kusomwa kwa Dua kabla ya kuaza kwa shughuli za Kikao cha Baraza leo
asubuhi.
Mhe. Mahmoud Thabi Kombo akiwashukuru wananchi wa jimbo la kiembesamaki
kwa mashirikiano yao tangu mwazo wa kampeni hadi kupiga kura na
kumchagua kuwa mwakilishi wao.
Picha Zote na Ramadhan Othman Mapara-Zanzibar
0 comments:
Post a Comment